July 4, 2021


 YANGA inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi, jana ilitibua sherehe za ubingwa wa Simba kwa kuichapa bao 1-0 mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu ambaye alikuwa uwanjani.

Ilikuwa ni dk 11 Yanga ilipata bao la ushindi kupitia kwa nyota wao Zawadi Mauya aliyepiga shuti kali akiwa nje ya 18 likagongana na Shomari Kapombe ambaye alimpoteza mazima mlinda mlango, Aishi Manula.

Jana Yanga walitibua sherehe ya ubingwa kwa Simba kwa kuwa ingepata sare ama ushindi ingetangazwa kuwa bingwa rasmi kwa msimu wa 2020/21 ila mambo yalikuwa magumu kwao.

Yanga inakuwa timu ya kwanza kuwatungua Simba baada ya mikoba hiyo kuwa mikononi mwake baada ya kuchukua kutoka kwa Sven Vandenbroeck ambaye alipoteza kwenye mechi mbili.

Jumla Simba inaoyoongoza ligi ikiwa na pointi 73 imepoteza mechi tatu na kote kichapo chake ilikuwa ni mwendo wa mojamoja.

Gomes aliongoza timu hiyo kwenye jumla ya mechi 14 bila kufungwa na mechi yake ya 15 jana alionja joto ya jiwe kutoka kwa Yanga iliyo nafasi ya pili na pointi 70 baada ya kucheza mechi 32 huku Simba ikibakiwa na pointi 73 baada ya kucheza jumla ya mechi 30.


Sasa Simba ikiwa inahitaji kusepa na ubingwa wake inapaswa kupambana kwenye mchezo wake ujao wa ligi mbele ya KMC unaotarajiwa kuchezwa Julai 7, Uwanja wa Mkapa.

Katika mchezo wa jana, Simba yenye Meddie Kagere, John Bocco na Chris Mugalu ilipiga jula ya mashuti mawili yaliyolenga lango huku Yanga ikipiga mashuti manne ambayo yalilenga lango.

Kwa umiliki wa jumla rekodi zinaonyesha kwamba Simba ilikuwa na asilimia 61 za umiliki huku Yanga ikiwa na asilimia 39.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic