July 15, 2021


 TUPO kwenye wakati wa lala salama ambapo asilimia kubwa timu zote zimebakiza mechi mbili kwa ajili ya kumaliza mechi zao kwa msimu wa 2020/21.


Matukio mengi yamekuwa yakitokea ndani ya uwanja na nje ya uwanja lakini yote kwa yote ni muhimu kuona ushindani ukiendelea mpaka mwisho wa ligi utakapofika.


Kikubwa ambacho kinatakiwa kwa kila timu kuwa na nidhamu kwa kuwa hapa tulipokutana niliweka wazi kwamba hakuna haja ya kwenda na matokeo kwa kuwa kila timu inahitaji ushindi.


Tayari bingwa wa ligi ameshatangazwa ambaye ni Simba baada ya kushinda mbele ya Coastal Union ile ya Tanga hivyo jalada la ubingwa limefungwa kwa msimu huu.


Inaonyesha kwamba Simba walikuwa wamedhamiria kutwaa ubingwa msimu huu kama ambavyo iliweza kuanza kwa kasi katika kupambania taji na imefanikiwa.


Hilo liwe darasa kwa wengine kuangalia wapi ambapo walikosea ili msimu ujao wawe kwenye ushindani wa kweli na kutimza malengo yao.

 Niliweka wazi kwamba muhimu kwa kila timu kujipanga kufanya vizuri katika mechi zao zijazo ili kuweza kuwa imara na kupata matokeo chanya.


Jambo la msingi kwa sasa ni kuona kwamba mipango iliyoanza kupangwa inatazamwa kwa mara nyingine ili kuona kwamba kama imeweza kutimia ama imefeli.



Pale ambapo ilishindikana kutimia basi ni muhimu kupanga upya na kuangalia ni wapi mambo yalikuwa magumu ili kuweza kuwa imara zaidi wakati ujao.


 Ngumu sana kufikia mafanikio ya soka ikiwa kunamambo ambayo yanakwenda tofauti na hesabu ambazo zipo kwa kuwa kuna timu hazipendi maendeleo ya mtu mwingine.

Jambo la msingi kwa sasa ni kukaa chini kwa kuwa mechi mbili ambazo zimebaki zinakwenda kutoa maamuzi kwa timu ambazo zitashuka daraja na zile ambazo zitamaliza ndani ya 10 bora.


Kuanzia timu husika ni lazima ichukue hatua kwa wahusika ambao wamefanya jambo hilo na kueleza sababu ya wao kufanya hivyo kisha adhabu ikatolewa. 


Kitu pekee ambacho kimeonekana kwa msimu huu ni ule ushindani mkubwa ambao ulikuwa upo kwa timu zote katika kudaka ushindi licha ya wengi kuongeza kasi hasa mzunguko wa pili.

Imekuwa ni kawaida kwa timu nyingi kufanya hivyo na hilo limekuwa ni tatizo kwa zile ambazo zinahitaji kumaliza ndani ya 10 bora kushindwa kutimiza malengo yao.


Maandalizi ya mzunguko wa kwanza kwa timu nyingi yalikuwa ni ya kawaida tofauti na yale ya mzunguko wa pili hili nalo linapaswa kutazamwa na kila timu ambayo ilikwama kufanya vizuri kwa msimu huu mzunguko wa kwanza ina kazi ya kufanya kwa wakati ujao .

Muhimu kila timu ijue kwamba ikishindwa kufanya vizuri kwenye mechi zilizobaki hakuna namna kushuka daraja kunawahusu na malengo yao ya kuwa ndani ya tano bora ama 10 bora yatayeyuka jumla.

Ukiachana na suala la mzunguko wa pili mada yangu ambayo ninahitaji kuzungumza siku ya leo ni huhusiana na ndugu yetu mwana michezo mwenzetu, Gerald Mdamu ambaye ni mzawa anayecheza Polisi Tanzania.


Nimekuwa nikimfuatilia kwa muda mrefu Mdamu tangu alipokuwa Mwadui FC, Biashara United na sasa yupo Polisi Tanzania ni kijana ambaye alikuwa na malengo makubwa katika soka.


Pia ni moja ya wale ambao walikuwa wanapenda kufikia malengo ambayo walikuwa nayo hivyo alikuwa anaishi ndoto zake na bado kwa sasa ana ndoto ambazo anahitaji kuzifikia ila kuna tatizo ambalo amelipata.

 Ajali ambayo wameipata wachezaji wa Polisi Tanzania inawahusu wanafamilia wote wa michezo huku ripoti za madaktari zikionyesha kwamba Mdamu ameumia zaidi.


Kuvunjika miguu miwili kwa mchezaji sio taarifa nzuri na kwa timu kupata ajali pia sio taarifa nzuri lakini kikubwa tunapaswa kujua kwamba tunapaswa kushukuru kwa yote.


Kwa kuwa Mdamu ni mwanafamilia mwenzetu katika ulimwengu wa michezo basi tuungane na Polisi Tanzania katika kumshika mikono ili aweze kurejea kwenye afya yake na majukumu ya kila siku.

Itapendeza kwa wakati huu kama ambavyo tulikuwa tukicheka naye katika nyakati za furaha basi wakati huu pia tuwe pamoja naye kwa kumpa sapoti kwa kutuma chochote kwa watu wa Polisi Tanzania.


Tusisahau pia kumuombea Mdamu pamoja na wachezaji wengine ambao walipata maumivu kwenye ajali hiyo ambayo imeacha maumivu kwa wengi hasa katika familia ya michezo.


Mdamu pole nyingi kwako kwa kuwa hakuna ambaye alikuwa anatarajia haya kutokea na maombi ya wanafamilia wengi ni kuona kwamba unarejea kwenye ubora wako na kuendelea na majukuu yako.


Kumshika mkono itapendeza na kumuombea pia ni jambo la msingi kwani yeye pia ni mwanamichezo mwenzetu na anapenda kurejea kwenye afya njema awe kama zamani.

Polisi Tanzania na familia ya michezo kiujumla tunatambua kwamba nyakati hizi ngumu kila mmoja anakuwa kwenye nyakati ngumu hivyo muhimu kutulia na kujipanga upya kwa mechi ambazo zimebaki.


Tumeona ujumbe ambao umetolewa na Polisi Tanzania kwamba tumshike mkono Mdamu, kwa kuwa tulikuwa pamoja kwenye furaha basi na muda huu tuwe naye pamoja katika huzuni ili baadaye tuwe naye tena kwenye furaha.

Kutokana na maombi ya familia ya michezo kuweza kumshika mikono nyota huyo ambaye amevunjika miguu yote miwili uongozi umeridhia ombi hilo na wale wanaotaka kumchangia watume kupitia namba 0713 898 446 Jina Frank Komba. 

 


 

2 COMMENTS:

  1. Huwe mkweli kwamba TFF wamelazimisha Simba awe Bingwa kwa kuweka ukiritimba kwenye ratiba na kuwandaa marefa wa kujiripua wakijua point tatu zitatoka na nitafungiwa mechi tatu au nitasakamwa bila kifungo eg Sasi nk. Kwamba mtajadili Makosa ya Refa lkn matokeo hayabadiriki.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic