July 15, 2021

 


KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassreddine Nabi, leo Julai 15 kimesepa na pointi tatu mazima za Ihefu FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila.



Ushindi wa mabao 2-0 umewatosha Yanga kusepa na pointi hizo katika mchezo wa leo ambao ulikuwa nj maalumu pia kumuaga nyota wao Haruna Niyonzima ambaye mkataba wake wa miezi sita umemeguka na hajaongezewa kandarasi.


Ni mabao ya kiungo Feisal Salum ambaye aliyafunga yote mawili ambapo lile la kwanza dk ya 17 na lile la pili dk ya 36.


Jitihada za Ihefu kuweza kuweka usawa mzani ziligonga mwamba na kufanya timu hiyo kupoteza jumla ya Pointi sita mbele ya Yanga.


Mchezo wa kwanza ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-0 Uwanja wa Sokoine na leo imepoteza kwa kufungwa mabao 2-0 Uwanja wa Mkapa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic