July 15, 2021


 TAYARI mashabiki wa Waliooa wameanza kupanga kikosi kazi chao huku wakiweka wazi kuwa kiraka wao Elvas Stambuli atafunga bonge moja ya bao watakapokutana Julai 30 dhidi ya Wasiooa ambao ni wafanyakazi wa Global Group.

Akizungumza kwa msisitizo mkubwa shabiki namba moja wa Waliooa, Bahati Haule ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Wasanifu kurasa alisema kuwa wanasubiri muda ufike wawape dozi ya maana wapinzani wao.

“Tuna wachezaji tegemeo na wenye uwezo wa kuamua matokeo, mabao yakipungua labda matatu na tutawafunga tunavyotaka, Mzee Stambuli yule atafunga na langoni hakuna atakayeweza kumfunga kipa namba moja Mgella, (Charles).

Kwa upande wa shabiki wa Wasiooa, Asha Kabuga mpiga picha na mhariri namba moja ndani ya Global TV alibainisha kuwa wameskia tambo zao watafanya kweli uwanjani.

Kwa Wasiooa wanapigwa tafu na Smart Gin na Creative Bee ambao watatoa jezi wengine ni Peak Time Media, Tukuyu Spring Water, Global TV na +255 Global Radio wameweka mkono wao wa nguvu huku kwa wale Waliooa wakipigwa tafu na Saleh Jembe Blog.

 Pia kwenye mchezo uliopita Waliooa wakiongozwa waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 Uwanja wa Sinza hivyo mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic