INAELEZWA kuwa klabu ya soka ya Juventus ipo tayari kumuachia staa wao Cristiano Ronaldo kujiunga na PSG, ili waipate saini ya staa Mauro Icardi.
Kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri ameweka wazi kuwa anahitaji huduma ya Icardi kwenye kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao, na mabosi wa Juventus wanapamabana kuinasa saini yake. Huku PSG wao wakiweka wazi kuwa wanamuhitaji Ronaldo.
Mfungaji huyo bora wa michuano ya Euro 2020 hivi karibuni aliweka wazi kuwa hataki kusalia ndani ya kikosi cha Juventus, licha ya kwamba mpaka sasa amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja kusalia ndani ya kikosi cha timu hiyo na kama ataenda PSG basi ataungana na Mbrazili, Neymar Junior.
Nyota huo ambaye ana miaka 36 kwa sasa anaonekana kukosa furaha ndani ya Juventus hasa baada ya kukosa ubingwa wa Ligi Kuu Italia msimu huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment