July 17, 2021

 UONGOZI wa Klabu ya Azam FC umebainisha kuwa hawajapata ofa yoyote kutoka Yanga inayomujitaji beki wao Yakub Mohamed.



Yakub raia wa Ghana amekuwa akitajwa kuingia rada za Yanga kwa ajili ya kutumika hapo msimu wa 2021/22.


Sababu kubwa za Yanga kuhitaji saini yake ni kumpata mbadala wa Lamine Moro ambaye amekuwa akisumbuana nao katika suala zima la nidhamu.


Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa hawajapata ofa yoyote kutoka Yanga na isitoshe mchezaji huyo ana mkataba.


"Hatujapata ofa yoyote kutoka timu yoyote kwa sasa hizo unazosikia ni tetesi, pia mchezaji bado ana mkataba na Azam FC,".


Chanzo: Championi.

1 COMMENTS:

  1. Yaani mtu Hana namba Azam ,vp aje Yanga yenye madefender wa Dunia eg Banuchi kweli umetukosea si aende Simba cse mwakani hamtabebwa na ratiba .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic