HABARI ikufikie kuwa uongozi wa Yanga
umeamua kubadili rasmi mipango ya kutua
nchini kwa wachezaji Shabani Djuma na Fiston Mayele ambao walitakiwa kutua mapema wiki
hii.
Yanga tayari ilikwishamalizana na Shabani
Djuma ambaye alikuwa ni beki wa kulia wa AS
Vita mara baada ya kumsajili kwa mkataba wa
miaka miwili huku Fiston Mayele yeye akikiri
wazi kuja kukamilisha dili na Yanga pindi
atakapotua nchini sambamba na Shabani
Djuma.
Chanzo chetu cha uhakika kutoka Yanga
kimeliambia Championi Ijumaa kuwa sababu
kubwa ya kubadili siku ya wachezaji hao kutua
nchini ni uwepo wa fainali ya Kombe la
Shirikisho la Azam Sports (ASFC) dhidi ya Simba
ambapo inaweza kuleta presha kwa wachezaji
ambao wapo kwa sasa, hivyo ujio wao utakuwa
mara baada ya kumalizika kwa fainali hiyo.
“Ilikuwa ni mipango yetu kuona wachezaji hao
wanakuja na kushuhudia mchezo wa fainali
dhidi ya Simba lakini tumeona itawaongezea
presha kubwa wachezaji ambao wapo kwani
kama ambavyo unafahamu kwa sasa ni mwisho
wa msimu, kuna mambo ya kuachana na
wachezaji na kuingiza wachezaji wapya.
“Hivyo baada ya kumalizika kwa mchezo huu,
tunatarajia wachezaji hao kuingia hapa nchini
kwa ajili ya taratibu mbalimbali za timu
ikiwemo mipango ya maandalizi ya msimu
ujao,” kilisema chanzo hicho.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa
Yanga, Dominick Albinus, alisema kuwa uongozi
wa klabu hiyo hautarajii kumpokea mchezaji
mpya yeyote ndani ya klabu hiyo kwa sasa
labda mpaka kumalizika kwa mchezo wa fainali
dhidi ya Simba mara baada ya ligi kumalizika.
“Ligi tayari ilishamalizika, kilichobaki kwa sasa
ni kumalizika kwa mchezo wa Kombe la
Shirikisho tutakaocheza dhidi ya Simba huko
Kigoma, ndio mambo mengine yaweze
kufanyika kwa kufuata taratibu maalumu
zilizoandaliwa na uongozi wa Yanga.
“Kuhusu wachezaji wapya kuja kuutazama
mchezo wa fainali dhidi ya Simba niseme
hapana hakuna mpango kama huo kwa timu
labda mpaka fainali hii itakapomalizika ndio
tunatarajia kuona wachezaji wapya wakianza
kutua nchini,” alisema kiongozi huyo.
Mnaweweseka
ReplyDeleteSawa kabisa
ReplyDelete