UNAKUMBUKA ile posho ya milioni 500 ambayo
uongozi wa Yanga uliwaahidi wachezaji na
benchi la ufundi endapo wataifunga Simba
katika mchezo wa Ligi Kuu na Yanga
wakafanikiwa kuifunga?
Sasa unaambiwa matajiri wa Yanga wameweka kiasi hicho hicho ili waifunge tena Simba katika mchezo wafainali ya FA itayochezwa kesho Julai 25, mkoani Kigoma.
Hivyo ramani ya Simba kufungwa imechorwa na mabosi kupitia mkwanja mrefu uliowekwa mezani ikiwa wataweza kuwafunga watani zao hao wa jadi.
Yanga katika mchezo uliopita dhidi ya Simba
walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0
katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu
Bara kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar, huku
mchezo wa safari hii katika fainali ya Kombe la
Shirikisho la Azam Sports ukitarajiwa kufanyika
katika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani
Kigoma.
Chanzo chetu cha ndani ya Yanga kimeliambia
Championi Ijumaa kuwa uongozi wa Yanga
umeweka ahadi kama waliyoiweka katika
mchezo ule wa kwanza ambao Yanga ilifanikiwa
kuibuka na ushindi wa bao 1-0 huku wakiamini
pia kiasi hicho kitatosha kuwapa motisha
wachezaji na kupata ari ya kupambana na
kuibuka na ushindi dhidi ya wapinzani wao.
“Uongozi wa Yanga umetoa ahadi kama ile ya
mwanzo ambayo ilisababisha Yanga iweze
kuibuka na ushindi dhidi ya Simba, kama
unakumbuka kiasi cha awali katika mchezo
uliopita ilikuwa ni milioni 500 jambo ambalo na
safari hii uongozi umeamua kuweka kiasi
hichohicho.
“Sababu kubwa ya kufanya hivyo kwa viongozi
wanaamini kuwa kiasi hicho kinatosha kuwapa
wachezaji ari ya kupambana na kuipatia ushindi
timu kama ambavyo ilivyotokea mara ya
kwanza ambapo Yanga ilifanikiwa kuibuka na
ushindi katika mchezo wa ligi,” kilisema chanzo
hicho.
Alipotafutwa Dominick Albinus ambaye ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga
alisema kuwa ahadi na posho za wachezaji na benchi la ufundi la Yanga kuelekea katika mchezo wa Yanga zinabaki kuwa siri kutokana na mambo mbalimbali ambayo yamekuwa yakijitokeza baada ya ahadi hizo.
“Kuhusu ahadi kuelekea mchezo wetu wa fainali dhidi ya Simba inabaki kuwa ni siri kati ya viongozi wa timu, benchi la ufundi na wachezaji kwani mara nyingi mara baada ya kutangaza ahadi mambo mbalimbali hujitokeza ambayo tumekuwa tukiyalaani sisi kama viongozi,” alisema kiongozi huyo.
Hoyo ndio ramani, nilidhani no tactics za uchezaji kumbe motisha. Sawa.
ReplyDeleteHiyo ndio mchoro. Na kiasi kidoogo alikula refa kuhakikisha anatibua kila move itayoweza kuleta madhara. Yupo mchezaji mmoja alikuwa anajua wapi refa anapatikana....... ila AA kidogo kuna mashaka simu yake haipatikani
DeleteWasikilizeni waandishi kama kawaida ya watu wenye mihemko ya mikia kupinda
ReplyDeleteWazee wa kuishia kuchora ramani ile ramani ya ubingwa iliishia wapi
ReplyDeletedirayamafanikio.blogspot.com
ReplyDeleteMchora ramani hakueepo kwenye ligi kuu?
ReplyDelete