July 25, 2021





MWAMUZI wa mtanange wa Yanga dhidi ya

Simba kwenye mchezo wa fainali ya michuano

ya Shirikisho la Azam (ASFC), Ahmed Arajiga,

amechezesha michezo miwili ya Simba ambayo

yote wameshinda na kufikia hatua ya fainali.


Timu hizo zinatarajia kushuka dimbani

leo Jumapili kwenye Uwanja wa Lake

Tanganyika, Kigoma ukiwa ni mchezo wa

kumtafuta bingwa wa michuano ya ASFC.


Takwimu zinaonyesha kuwa mwamuzi, Arajiga

ni faida kwa Simba ambapo kwenye michezo

miwili ya ASFC aliyochezesha ambayo ni ya

Robo fainali na Nusu fainali, Simba

wameshinda.


Mchezo wa kwanza ulikuwa dhidi ya Dodoma

Jiji uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini

Dar ambapo Simba waliibuka na ushindi wa

mabao 3-0, mchezo uliopigwa Mei 26, mwaka

huu.


Mchezo wa pili ulikuwa dhidi ya Azam FC,

uliopigwa Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja

wa Majimaji, Songea ambapo Simba iliibuka na

ushindi wa bao 1-0.


Mwamuzi huyo mwenyeji wa mkoani Manyara

hajachezesha mchezo wowote wa Yanga kwenye michuano ya Shirikisho la Azam kwa

msimu huu. 

Kuhusu suala la mwamuzi huyo, Yanga waliandika maoni kwamba uteuzi wa mwamuzi huyo wanaona kama hawajauelewa kwa kuwa amechezesha mechi nyingi za wapinzani wao.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi Tanzania, Sud Abdi alitoa taarifa kwamba sababu mojawapo inayofanya waweze kumteua mwamuzi ni pamoja na mechi ambazo amechezesha uwezo wake pamoja na vigezo vingine ambavyo wanazingatia.

Hata Ulaya amebainisha kuwa huwa wanafanya hivyo kwa kumchukua mwamuzi kulingana na mashindano amechezesha katika mashindano husika.

14 COMMENTS:

  1. Ungesema hiyo faida inakujaje .... Nyie waandishi nadhani hamjielewi na pia Kama hamjui hii habari ni ya kichochezi kbs

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwani wewe hujui kua hua anawabeba simba na aliwabeba nusu fainali walipocheza na Azam !! mbona kila kitu kilikua wazi rudia clip za mchezo uone mwenyewe !!

      Delete
    2. Tatizo lenu mmekariri,angalia mechi ya mwisho ya simba,na kwa mtazamo wako basi hata ile atakua amebebwa maana alianzisha mpira kwa haraka baada ya kuchezewa faulu na goli likafungwa mpira ukawekwa kati,acheni kukariri wapendwa.

      Delete
    3. ile mechi ya nusu fainali na Azam....ile faulo imeishajadiliwa Azam TV baada ya mechi, mwl kashasha na kipyenga cha mwisho wote wamesema mwamuzi alikuwa sahihi...mechi ya mwisho simba na namungo mbona faulo imechezwa na simba wakapata goli...haruna Niyonzima aliishaanzisha mpira kama ule Yanga wakashinda kagame cup..mbona pale sio tabu..Haya tuambieni refa aliyechezesha Simba na Yanga jul 3 alichezesha kihalali?

      Delete
    4. Jul 3, ulitaka BOCCO wampe kad nyekundu????

      Delete
  2. Naona muandishi anataka kutuaminisha kuwa huyo muamuzi huwa anaibeba simba. Uandishi wa aina hii sio wa kufumbia macho maana inaweza kuwa chanzo cha uchochezi. Unasemaje muamuzi ni faida kwa timu wakati mechi haijachezwa? TFF msimfumbie macho huyu muandishi

    ReplyDelete
  3. Timu nyingine hazina tofauti na vikundi vya wacheza singeli

    ReplyDelete
  4. Kuna watu wamegundua uwezo wao mdogo sasa wanataka kutumia mbinu zisizo halali, leo hatoki mtu

    ReplyDelete
  5. MAKANJANJA MAKANJANJA MAKANJANJA kawaambieni waliowatuma kuwa safari hii mambo magumu

    ReplyDelete
  6. Watu wa yanga hamjielwi kwa kweli, bas kama ni tafuteni na nyie Refa wenu wa kuwabeba,, Hakuna siku hamsemi wamebebwa?? Sasa km wamebebwa wangebewa kwenye ligi misimu minne mfululizo,, nyie mkiachwa kuimba wamebebwa, kwel ni wanayanga ni Manyani FC

    ReplyDelete
  7. Huyu mwandishi kibaraka bna unalipwa sh. Ngapi

    ReplyDelete
  8. Tatizo lenu mmekariri,angalia mechi ya mwisho ya simba,na kwa mtazamo wako basi hata ile atakua amebebwa maana alianzisha mpira kwa haraka baada ya kuchezewa faulu na goli likafungwa mpira ukawekwa kati,acheni kukariri wapendwa.

    ReplyDelete
  9. Zikitokea timu nyingine 5 kwenye ligi kuu bara zikawa na mawazo Kama ya Utopolo basi ligi haitachezeka maana kila siku itakuwa lawana za kijinga na kesi zisizo na mashiko

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic