July 25, 2021


BAADA ya Ofisa wa Habari wa Simba, Haji

Sunday Manara, kuweka hadharani chuki

anazodaiwa kufanyiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu

(CEO) wa timu hiyo, Barbara Gonzalez,

hatimaye uongozi wa Simba umetoa tamko.


Sauti iliyosambaa mitandaoni ambayo inadaiwa

ni ya Manara, ilisikika ikisema:“Barbara una chuki mbaya sana kwangu hadi naogopa kula mbele yako, naacha hii timu kwa ajili yako kwa sababu ya chuki yako kwangu, unajiona wewe ni Simba kuliko wote, unataka umaarufu kinguvu.


“Unadhalilisha wafanyakazi wa Simba na

kuwatishia, unatamani kuniondoa Simba,

sitakubali na hujui lolote kuhusu hii klabu,

subiri hii mechi ipite.


“Nasingiziwa eti nilienda Kigamboni kwenye

kambi ya Yanga, vitu vya hovyo kabisa, mimi

sinunuliki kwa thamani ya fedha Barbara

kwangu haya ni matusi.”


Baada ya maneno hayo kuzuka, Championi

lilimtafuta mwenyekiti wa Simba, Murtaza

Mangungu, ili azungumzie ishu hiyo ambapo

alisema: “Tunasubiri mechi ya Kigoma iishe ndipo

tuweze kuongea nao na kutatua tatizo ila kwa

sasa tumeweka akili zetu kwenye mchezo wa

Kigoma.


“Suala la wao kwenda Kigoma au kutokwenda

waulize wenyewe watakujibu.”


Jumapili hii Simba itakuwa ikicheza na Yanga

kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho kule

Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.



5 COMMENTS:

  1. Ovyo kabisa utazani matoto kumbe watu wazima

    ReplyDelete
  2. Sakata la KHAJI MANARA, Barbara anaingia vipi Mbona mnapotosha Umma.Sakata la Barbara kwani ipo sehemu alisikika akishiriki katika ugomvi?

    ReplyDelete
  3. Mbinu chafu ya kuitoa Simba ktk mstari ndio imefeli sasa chukueni Manara na Mzee Mpiri ili muijenge Club yenu.

    ReplyDelete
  4. Simba team kubwa Ina taratibu na misingi ya kutatua matatizo lkn siyo km hivyo kuruka kwenye media lkn na Imani yote yatakuwa sawa kwani kupishana ktk kazi ni swala la kawaida na ndo kazi inapata samani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic