July 23, 2021

 HANS Poppe Zakaria, Mwanachama wa Klabu ya Simba amesema kuwa hajapendezwa na tabia ya Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kusikika akimlalamikia Mtendaji Mkuu wa Simba,  Barbara Gonzalez. 



Hivi karibuni imekuwa ikisambaa sauti ya Manara ikidai kwamba anachukiwa na Barbara ambaye amekuwa akiwadhalilisha wafanyakazi.  Pia ilienda mbali sauti hiyo ikaeleza kuwa Manara anafanya kazi kubwa bila mkataba na analipwa laki 7 kwa mwezi.

Sakata hilo limezidi kuwa la moto ambapo Manara kupitia mitandao ya kijamii amesema kuwa baada ya mchezo dhidi ya Yanga kuisha ataongea kwa kuwa sauti ambazo zinasambaa kwa sasa ni za muda mrefu.

Hans amesema kuwa kitendo cha Manara sio kizuri hasa kuelekea kwenye mchezo mgumu dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Julai 25, Uwanja wa Lake Tanganyika na amebainisha kuwa alipewa mkataba wa milioni 4 bado hajasaini.

"Kitendo ambacho amekifanya Haji sio kizuri na sijakipenda hata kidogo hasa kwa kumfanyia bosi wake. Nipo ndani ya Simba na ninajua kwamba kuna miiko ya kazi lakini kwa Manara amefanya jambo ambalo halipo katika miiko.


"Labda anaona kwamba yeye ni mkubwa kuliko Simba hiyo sio sawa lazima amuheshimu bosi wake na kuna utaratibu wa kufanya katika mambo kama haya pale yanapotokea.

"Nimeskia analalamika kuhusu mshahara wa laki 7 basi aseme kuhusu mkataba wa milioni 4 ambao amepewa ili asaini, mbona amepewa muda mrefu na hajasaini kwa nini?.

15 COMMENTS:

  1. Tusubir mechi ipite kwanza

    ReplyDelete
  2. Huo hapo juu ndio ukweli. Manara ni kipenzi wa mashabiki na msemaji ws babu kubwa hakuna aliyemuweza. Hauwezi kumtaja Manara bila ya kuitaja Simba wala kuitaja Simba bila ya kumtaja Manara. Ilitusikitisha Kwa mtu kama yeye kuyafanya aliyofanya pamoja na kuingia mitandaoni. Naamini binaadamu hupitiwa lakini kwa mtu kama Manara dikutegenea

    ReplyDelete
  3. Kujijenga inachukuwa miaka lakini kukjibomoa ni dakika. Manara keshajiharibia

    ReplyDelete
  4. Imeshaamuluwa kuawa refa ni yuleyule waliemkataa na kilichobaki ni kuota mbawa

    ReplyDelete
  5. Hivyo Manara anashindwa kufahamu kuwa maagizo na ushauri wa CEO ni maagizo ya taasisi? Kuna wapumbavu fulani wanasema ooh Manara hakuwa anaidhalilisha taasisi Bali ni ugomvi wa Kati ya mfanya kazi na mfanya kazi.Jamani? Naomba radhi kwa hiyo lugha nilioitumia lakini wanahabari ni waelimishaji sio wa po to sha ji. Barbara sio mtu alietoka from nowhere kuja Simba. Barbara ni miongoni mwa wadada wakujivunia watanzania.Shes very proffesional kwenye majukumu yake ya kazi ila watanzania wengi hatujazoea kusimamiwa kufuata taasisi inataka nini. Tumezoea kujifanyia mambo ya kazi tunavyotaka sisi wenyewe. Watanzania wengi tunaoishi nje tumebakwi na mshangao kuwa mfanyakazi wa kawaida anamtukana CEO wake halafu bado anakuwa na jeuri ya kuendelea kutamba mitandaoni. Kwanza ni kosa la jinai kumtishia mtu usalama wa maisha yake Kama alivyoahidi Manara kuwa atamfanyia Barbara kitu kibaya.Vyombo vyetu vya usalama hawaoni kuwa kauli za Manara zinatishia usalama Barbara? Manara anajinasibu kuwa muislamu safi? Muislamu safi anashindwa kuzizuia hasira zake kwa mambo waliongea faragha baina ya watu wawili anakwenda kulipuka m
    Kwenye kadamnasi ya umma? Wahenga wanasema debe tupu haliachi kupiga kelele na ukimya sio uoga ni ujasiri uliokamilika.

    ReplyDelete
  6. Bugatt mmjatu tacc nzima umeichanganya daah weekweli nimtu na nusu nakubali Kaka

    ReplyDelete
  7. Manara kaza kamba mpka barbra akuhonge yale mambo yetu hahahah

    ReplyDelete
  8. Tukiwaambia manara anaropokaga mnabisha na kumsifia ayafanyayo sasa yanawaumaaaaa maana amemtukana demu mwenye timu yao

    ReplyDelete
  9. Manara kajimaliza mwenyewe. Kajipoteza mwenyewe na kujiondoa kutoka kwakila aliyekuw anamuona hiro wa Simba. Hsta ingekuwa kwelu Barbara kskosea basi ilibidi yamalizwe kimyakimya, lakini mtu mkubwa kama huyu kujianika mitandaoni na kutaja mshahara wake na kuanika siri. Kajimaluzza na hapana ataempa pole ua rafiki yake Mzee Mpili na huku Yanga hawatski kumuona kwa jinsi alivojijengea uadui nao. Inaonesha cheo CEO cha Barbara akikitaka yeye

    ReplyDelete
  10. huyo Barbra ni chakula Mo hicho na ndiomana alimwambia Haji kuwa Simba ni yake yeye na Mo Haji yeye hausiki hahahahaaaaaa

    ReplyDelete
  11. Haji hana akili anaifanya simba ni yake, aondolowe tu mjinga huyu, kenge kabisa

    ReplyDelete
  12. Inawezakana keshafunguliwa mlango pale pahala ili awe msemaji mkuu kwasabsbu anazijuwa siri kwakuwa aliaminiwa

    ReplyDelete
  13. Nyie hamjui kitu. Manara ni remote inayoendeshwa na GSM. Ndio maana Haji hatoki Kigamboni kupata vibahasha kwa kazj ya kutoa taarifa za Simba. Yanga bhana ndio Wanyanchi. Marefa. Hujuma. Ushindi mezani. Lakini ikigika kimataifa ni vipondo tu

    ReplyDelete
  14. Manara akishaondoka basi huko anapojioekeka nao watamtimua kama paka meizi kwasababu nsko pia atawauza na kusahsulija kabisa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic