Na Saleh Ally
UKIACHANA na suala la kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara nne mfululizo katika kipindi hiki, moja ya sifa kubwa kabisa ya Klabu ya Simba ni uongozi unaofuata weledi.
Simba ndio mfano wa uongozi kwa klabu nyingine, kwamba wanaendesha mambo yao kwa kufuata utaratibu sahihi kabisa kulingana na ubora wao.
Kweli kikosi chao ni bora, mambo yao yanaonekana yanakwenda kwa utaratibu mzuri kabisa katika kipimo sahihi na kila kitu ni kizuri.
Wengine wanapaswa kuanza kuiga au wameanza kuiga kutokana na wanavyosikia namna ambavyo Simba inaendeshwa. Kitu kizuri ni chachu ya mabadiliko na baadaye mafanikio kwa wengine.
Kwa sasa, mambo yanaanza kwenda tofauti na huenda ikaamka picha mpya kwamba inawezekana hata kwa watu wanaojitambua na kuendesha kazi zao kwa ufasaha kuanza kulumbana hadharani.
Kuna sauti ambayo imeanza kusambaa usiku wa kuamkia juzi, ikisikika Msemaji wa Simba, Haji Manara akimshutumu mambo kadhaa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez.
Maneno ni mengi na inaonekana katika shutuma hizo, Manara analia kudharauliwa, kunyanyaswa na kufanyiwa roho mbaya huku akisisitiza kwamba atazungumza baada ya mechi dhidi ya watani wao wa jadi Yanga kule Kigoma, Jumapili.
Manara ameendelea kueleza anavyokerwa na mambo kadhaa huku akitupa shutuma lukuki kwa Barbara ambaye ameendelea kuwa kimya.
Mchana kwenye ukurasa wake wa Instagram, ameeleza kwamba aliyevujisha sauti ile ni Barbara mwenyewe kwa kuwa yeye ndiye alimtumia. Akasisitiza aliamini anazungumza naye huku akiwa amejipanga kuzungumza baada ya mechi hiyo ya Kigoma, lakini sauti hiyo imevujishwa kwa makusudi.
Hilo ndiyo gumzo kubwa zaidi katika mchezo wa soka, wakati watu wanakwenda katika fainali ya Kombe la Shirikisho mjini Kigoma, sura imekuwa tofauti na sasa ni Manara wa Simba dhidi ya Barbara wa Simba. Jiulize!
Vipi iwe viongozi wa Simba walumbane katika kipindi kama hiki ambacho unatarajia kuiona timu hiyo ikijipanga vizuri kwa ajili ya kushinda mchezo huo?
Kati ya maneno aliyoyazungumza Manara ni kuhusiana na yeye kutuhumiwa kwenda kwenye kambi ya Yanga huku akisisitiza anadhalilishwa na bosi wake huyo ambaye amemuita ni anayependa umaarufu.
Yanga kwao wanaona ni kama hasira za mkizi au vita ya vifaranga vya kuku inayokwenda kuwa faida kwa kunguru au mwewe, jambo ambalo kwa Simba linawapitisha katika sifa mbovu kabisa.
Katika yale maneno, Manara mwisho
alimaliza kwa kumueleza bosi wake huyo
mwanamama “koma”. Lile neno
linalomsisitiza mtu kuacha au kuachana
na jambo fulani. Nami niwasisitize
kwamba iwe hadharani au chinichini,
bado wote hawakupaswa kuonyesheana
nani zaidi kwa kipindi hiki.
Tunamuona Barbara akiwa
amenyamaza, lakini kwa mujibu wa
Manara alimshambulia kwa maneno
kadhaa ambayo yanaonekana kumkera
na kuanzisha mjadala huo ambao binafsi
nauona hauna manufaa kwa Simba kwa
kuwa wao wote wawili ni waajiriwa wa
Simba hata kama ni kweli Barbara
alisema yeye ndiye mwenye Simba kama
alivyosema Manara. Kama viongozi ambacho walipaswa kukiangalia ni maslahi mapana ya kikosi
cha Simba na Wanasimba
wanaoizunguka klabu hiyo. Ikishinda ni
faraja kubwa sana kwao na ikipoteza ni
maumivu makubwa, sasa vipi waingize
jambo linalopoteza mwendo wao
unaopelekea umoja na mafanikio
ambayo yamewapa sifa.
Sifa ya weledi inapotea, sifa ya uongozi
bora kwao inapotea na hata lile jambo la
kushindwa kwamba wanapaswa
kulumbana wakati gani basi ni shida
nyingine kubwa na litakuwa jambo bora
wakikaa kimya, baadaye
wakakutanishwa na ikiwezekana
kuyaweka mambo sawa na waendelee.
Simba inaongozwa na watu ambao ndio
wawakilishi wa kikosi chao. Dhamana
waliyopewa ni kubwa sana, asiwepo
anayeona ni zaidi ya mwingine, asiwepo
atakayeona ni mkubwa kuliko klabu au
bora sana zaidi ya wengine. Ikiendelea
hivyo, watapoteza uelekeo na kuna siku,
watashangaa kuona walipo ni chini ya
wengine.
Kama kuna mgogoro, mazungumzo
hayajawahi kushindwa na kama ni chuki
za mioyo baina yao, basi kuna viongozi
wanaoweza kufanya wakayamaliza lakini
kwa kilichotokea, badala ya kuishia kwa
Manara au Barbara kinaiangusha Simba
yenyewe kuonekana imefeli kiuongozi.
Wote wawili mkome!
Kuweni makini na uandishi wenu.... Malumbano ni pale ambapo pande mbili au watu wawili kurushiana maneno, lakini mpaka sasa si Barbra wala uongozi wa simba waliojibu shutuma za manara hivyo kilichopo sio malumbano ila ni malalamiko toka kwa manara
ReplyDeleteMimi naona Kama Waandishi tunarudi pale alipoanzia Manara "takataka" uweledi upo wapi kwenye kazi ya uandishi wa habari? Lengo hapa ni kuona haya mambo ya Manara yanakuzwa zaidi katika kuichafua Simba nzima. Tangu clips hizo za Manara zitoke hakuna sehemu ambayo Barbara kasikika akibishana na Manara.Sasa mnaolazimisha kusema ni malumbano kati ya Barbara na Manara aidha ni vilaza wa ufahamu au ni wanaume wenye tabia ya kudhalilisha wanawake ila kwa hili hapa Barbara hatendewi haki mwenye matatizo amejitanaza mwenyewe kuwa yeye ndie mwenye na kuahidi kusambaza clips hizo kwa kila mwanasimba,sasa vipi leo mnalazimisha kumuingiza mtu mwengine asiehusika?
DeleteNadhani hapa tunapaswa kumpa kila aina pongezi mwanadada huyu kwa kuwa imara na jasiri katika kipindi chote hiki kigumu kwakukaa kimya na kujikita zaidi katika kupambana kuhakikisha kuwa timu yake inafanya vizuri kwenye mechi ya Jumapili. Barbara ameonesha kuwa kweli Simba hawakukosea kumpa ule wadhifa. Kiongozi imara anaoneka katika kipindi Cha misukosuko na Barbara anatuonesha sasa kwa vitendo, pongezi sana Dada.
Mmesema barbra amekaa kimya sasa mnasemaje malumbano
ReplyDeleteJapo mimi siyo mwanasimba, katika hili sikuungi mkono! Haiwezekani CEO wa Simba umuweke kwenye kariba moja na Mkuu wa Kitengo, halafu uwaambie "wote wawili mkome?" Ndivyo inavyokuwa!
ReplyDeleteHaji kafikishwa hapo na uwezo wake duni wa kuchuja nini aseme nini astahimili. Kuropoka na kubwabwaja kwake ni kawaida na sasa tangu aanze kubaki na salio "ashaanza kuwa jeuri na kibri", aliwahi kutaka kuwarudishia pesa wanayanga waliomchangia akapate matibabu ya macho, aliwatukana waandishi hadharani, alimtukana Mkude sasa kawa kidume anamdindishia boss wake?...anadhani mitandao itamsaidia kubaki salama?
Kwa uzoefu wangu wa uongozi, ukishamuona boss kanyamaza, ujue umuemia!
Huyu mama ni msomi, mwenye uwezo wa hali yajuu katika kutimiza wajibu wake na vilevile uwezo wa kuendana na watu wa tabia mbalimbali, huyu sie wale wa kuropokwa au kuzozana. Kaijenga Simba na ndio imetulia katika ahadi zake na hayo ndio yonayowaumiza wengine
ReplyDeletehttp://dirayamafanikio.blogspot.com/2021/07/umechagua-kuwa-mshindi-au-mshindwaji.html?m=1
ReplyDeleteKwani wakati Haji Manara mwenyewe anadai atatuma clip ile kwa watu wote alimaanisha nini? Au akili zake ni maji kupwa maji kujaa? Au anadhani sote tu wasahaulifi?
ReplyDeleteAlifikiria sana kuwa Simba bila take hakutokuwa na Sinba ya leo na alitikisa kibiriti akifikiri uma utakuwa nyuma yake lakini mwishoni alitambuwa alipaa kwa kupaishwa na Simba na kujikuta keshapoteza imani ya wana Simba na maji yakimwagika hayazoleki tena
ReplyDelete