July 24, 2021


 LICHA ya kukamilisha mzunguko wa pili na kucheza jumla ya mechi 34, safu ya ushambuliaji wa Simba inayoongozwa na John Bocco imeonekana kuwa kwenye makali yaleyale ya msimu wa 2019/20 bila kupoa.


Wakati ikitwaa taji la ligi msimu uliopita baada ya kucheza jumla ya mechi 38, Simba ilifunga jumla ya mabao 78 na kinara wa utupiaji alikuwa ni Meddie Kagere ambaye alitupia mabao 22.


Msimu huu wakiwa wamecheza mechi pungufu ya nne kufikia 38, safu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, raia wa Ufaransa imetupia mabao yaleyale 78 kibindoni na kinara wa utupiaji ni Bocco mwenye mabao 16.


Pia rekodi nyingine ambayo safu ya ulinzi imeweka ni kuruhusu mabao machache ambayo ni 14 tofauti na msimu uliopita ambapo ilikubali kuokota jumla ya mabao 21 nyavuni.


Rekodi pekee ambayo imekuwa ngumu kwa Simba kuvunja ni ile ya kufikisha pointi 88 kwa kuwa msimu huu imekusanya pointi 83.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic