KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa kipindi cha kwanza walicheza vibaya mbele ya Yanga jambo ambalo lilifanya wakafungwa mapema.
Julai 3 itabaki kwenye rekodi ya Gomes pamoja na Simba kiujumla kwa kupoteza mchezo wao wa ligi mbele ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.
Gomes amesema kuwa walishindwa kucheza vizuri kipindi cha kwanza na walicheza vibaya jambo lililowafanya washindwe kupata ushindi.
"Ninasikitika kupoteza mchezo mbele ya wapinzani wangu Yanga kwani sikutarajia kuona matokeo ya aina hiyo kwa wachezaji wangu pamoja na timu kiujumla.
"Ila kwa kuwa tumepoteza hakuna namna tutajipanga kwa ajili ya mechi zijazo ila ukweli ni kwamba ninastahili lawama zote mimi ninazibeba licha ya kwamba wachezaji walicheza vibaya.
"Kipindi cha kwanza ambapo tulifungwa mapema tulicheza vibaya na wachezaji wangu walitengeneza nafasi walishindwa kuzitumia hivyo ninasikitika kweli," amesema.
Kwenye msimamo Simba ipo nafasi ya kwanza ina pointi 73 huku Yanga ikiwa nafasi ya pili ina pointi 70.
Yanga imecheza jumla ya mechi 32 huku Simba ikiwa imecheza jumla ya mechi 30 inasaka pointi tatu ili kuweza kutimiza lengo la kuwa mabingwa wa ligi mara ya nne mfululizo.








Mzee mpili alikuwa amewafunga miguu na akili wachezaji wa simba, hata kigoma kama hamtajipanga kwa hili la nguvu za giza mtaendelea kufungwa na timu isiyo na uwezo
ReplyDeletenjoon na zile paka tu hakuna namna, au mkampokee ule uchawi wenu yule aliyekuja na miguu toka kigoma, afrika nzima inajua simba wanga
DeleteWao wanaona wana uwezo kimpira
Deletekwa vile ni vyura wa kihansi wenye kuzaaa
Hiyo kigagula wenu mzee mpili sio mwanga? Mnamtumia vipi hapo, au ana cheo kipi
ReplyDeleteUtopolo wachawi tu ndo maana mmeishia kuwa wa mchangani
ReplyDeleteSiku zote Simba huwa mnaona nyie ndo wenye haki ya kushinda,akishinda mwingine uchawi,kubalini kwamba mlizidiwa mbinu.
ReplyDelete