July 30, 2021

 


KAMPUNI ya Euromax wanaotengeneza kinywaji cha Smart Gin na Kampuni ya Creative Bee kwa pamoja wamekabidhi jezi za mchezo wa walioa na wasioa unaotarajia kupigwa leo Ijumaa kwenye Uwanja Sinza, Dar.

 

Kinywaji cha Smart Gin na Creative Bee ndiyo wamedhamini mchezo huo kwa upande wa vifaa vya michezo kwa wafanyakazi wa Global Group ambao wanaunda timu za Walioa na Wasioa.


Jezi hizo za timu zote mbili zimekabidhiwa jana katika kipindi cha michezo cha Krosi Dongo kinachorushwa mubashara na +255 Global Radio na Global TV Online.

Mwakilishi wa Smart Gin katika tukio hilo, Peter Kinabo alisema kuwa sababu iliowafanya waingie kwenye mchezo huo ni kutaka kutoa sapoti kwa timu ya wasioa kuelekea kwenye mchezo huo.


“Sisi kama Smart Gin katika mchezo huu tumeamua kuwasapoti upande wa walioa na ndiyo tumewaletea jezi ambazo watatumia kwenye mchezo wa Ijumaa pale kwenye mchezo husika.

“Lakini kuhusu Smart Gin ni kinywaji chenye kileo na kwa sasa tupo kwenye promosheni boxi jipya ambalo lipo na chupa 15 ambalo bei yake ni Sh 27,000 na boxi la Sh 54,000 ambalo linakaa chupa 30 kwa mawakala wetu wote,” alisema Kinabo.


Kwa upande wa Meneja Mkuu wa Creative Bee, Bakari Khatibu alisema kuwa wao kama Creative Bee wameamua kuwapendezesha upande wa Wasioa kwa kuwapa jezi kali ambazo zimekamilika kila kitu kuelekea kwenye mchezo huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic