July 15, 2021


 WAZIR Junior, mshambuliaji wa kikosi cha Yanga amesema kuwa bado malengo yake ya kuwa mfungaji bora hayajayeyuka kwa kuwa anaamini ana nafasi ya kufanya vizuri.

Ndani ya Ligi Kuu Bara, Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ikiwa imetupia jumla ya mabao 50 baada ya kucheza mechi 32 yeye ametupia mabao mawili.

Bao la kwanza alifunga Uwanja wa CCM Kirumba mbele ya KMC na bao la pili alifunga mbele ya Mwadui FC.

Akizungumza na Saleh Jembe, Wazir amesema kuwa bado ana malengo ya kuwa mfungaji bora kwa kuwa kuna mechi za kucheza na waliofunga mabao hawajafikia mabao 20.

"Ukitazama msimu uliopita nilifunga mabao 13 nilipokuwa Mbao, bado sijakata tamaa kuhusu kuwa mfungaji bora.

"Msimu huu ukitazama anayeongoza kwa mabao amefunga mabao 15 hivyo bado nina nafasi ya kuwa mfungaji bora na sijakata tamaa, kwenye mechi hizi mbili ambazo zimebaki nina amini kuna jambo nitafanya," amesema.

Kinara wa mabao kwa sasa ni nahodha wa Simba, John Bocco ambaye ametupia mabao 15 na nafasi ya pili ipo mikononi mwa Prince Dube mwenye mabao 14 huku Chris Mugalu wa Simba yeye ametupia mabao 13.

5 COMMENTS:

  1. Mnaandika upupu gani huu na nyie Kama mmekosa cha kuandika kaeni kimya

    ReplyDelete
  2. Daaah kweli ukiitwa Utopolo pigana aisee maana sio kwa ushuzi huo

    ReplyDelete
  3. Tunapindua meza kibabe hata ubingwa wa ligi kuu tunachukua subirini tar 23 muone tukitangazwa

    ReplyDelete
  4. Kuanzia Leo ndugu Salehe Mimi nitatekeleza lile wazo la kwamba hata ukiona habari uc comment maana hulazimishwi Ni hiali ,wewe Nia yako apangwe yeye tusipate matokeo maana Ni average player na hii habari KakA Ni la mmetunga au mnamsaidia huyo apangwe.

    ReplyDelete
  5. Cjawah kutukana ila naanza leo _ mwaandshi we n K kubwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic