July 15, 2021


 KOCHA Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa nyota wake wawili ambao ni mabeki, Virgil van Dijik ambaye aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Everton na Joe Gomes wapo vizuri.

Klopp amesema kuwa tayari mabeki wake hao ambao ni tegemeo kikosi cha kwanza wameanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao.

Ikumbukwe kwamba mabeki hao wamerejea uwanjani baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda wa msimu mmoja na nusu kwa kuwa walikuwa wakiuguza majeraha waliyoyapata mwanzoni mwa msimu huu.

Klopp amesema:"Virgil na Joe hao hawatafanya mazoezi mara mbili kama ilivyo kwa wenzao kwa sababu bado wanaangaliwa na madaktari.

"Lakini mpaka sasa wako vizuri japo sijui katika wiki nne zijazo watakuwa wamepiga hatua kiasi gani," .  

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic