July 15, 2021


 MSHAMBULIAJI wa Manchester United, raia wa England, Marcus Rashford anatarajiwa kukaa nje ya uwanja mpaka Oktoba akijiandaa kufanyiwa upasuaji wa bega.

Nyota huyo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa bega muda wowote kuanzia sasa hivyo hataonekana ndani ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu.

Tatizo la bega kwa nyota huyo lilianza kumsumbua tangu mwaka jana lakini hakuweza kufanyiwa upasuaji kwa mujibu wa vipimo ambavyo amefanya hivi karibuni ameambiwa kwamba anatakiwa kufanyiwa upasuaji ili apewe matibabu ya haraka.

Ikiwa itakuwa hivyo nyota huyo atazikosa mechi tisa ndani ya Ligi Kuu England na tatu za Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu huu wa 2021/22.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic