July 13, 2021


 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba kuelekea kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba, wataipiga kwenye mshono ambao waliwashona walipokutana Uwanja wa Mkapa.

Ikumbukwe kwamba Julai 3, Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 0-1 Yanga ulikuwa ni mchezo wa  ligi na mtupiaji alikuwa ni Zawad Mauya.

Wanakwenda kukutana kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho, Uwanja wa Lake Tanganyika ikiwa ni mchezo wa fainali, Julai 25.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz alisema kuwa wanakwenda kuwapiga wapinzani wao palepale kwenye mshono.

“Tulikutana nao Uwanja wa Mkapa bila wachezaji wenye majina tukaamua mchezo kupitia Mauya, sasa tunakwenda kuwapiga palepale kwenye mshono.

“Hamna namna sisi hatusemi sana ila tunatenda, tunajivunia mashabiki wetu ambao wapo pamoja nasi kila wakati, wadhamini wetu GSM pamoja na kazi kubwa ambayo inafanywa na Waandishi wa Habari kufikisha taarifa basi tukutane Kigoma,” alisema Nugaz.

5 COMMENTS:

  1. Mtaongea mengi mwaka Kama tuliwapiga 4 Kama hivi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hatutakubali wautatue mshono wetu tena

      Delete
  2. Huyu jamaa Nugaz inaonekana hata akilala ndoto zote ni Simba tu

    ReplyDelete
  3. Utopolo itamaliza ligi ikiwa unbeaten, piga kifuani Mara tatu Kisha sema utopolo bingwa 2020/21

    ReplyDelete
  4. Hahahaaa Yanga haina tabia ya kusema sana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic