July 30, 2021



NYOTA Mukoko Tonombe kiungo wa Yanga amepigwa faini ya shilingi laki tano kwa kosa la kumpiga kiwiko mshambuliaji wa Simba, John Bocco kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Julai 25.


Pia Mukoko amefungiwa mechi tatu kwa kosa hilo ambalo aliliafanya na alionyeshwa kadi nyekundu ya jumlajumla.

Pia taarifa imeeleza kuwa kipa wa Yanga, Farouk Shikalo amepigwa faini ya laki tano kwa kosa la kukwepa kusalimiana na wachezaji wa Simba pamoja na waamuzi jambo ambalo ni kinyume cha kanuni.

 

 Naye Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amepigwa faini ya laki tano kwa kosa la kugoma kuhudhuria mkutano wa Waandishi wa Habari.

Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kutokana na kikao cha Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kilichokutana Julai 27.

Pia Simba imepigwa faini ya shilingi milioni mbili kwa kosa la viongozi na mashabiki kukaidi maelekezo na kuanzisha vurugu  kwa kulazimisha kuingia mlango usio rasmi na shilingi laki tano kwa kosa la viongozi kuingia uwanjani kwa mlango usio rasmi.



Adhabu nyingine ilikuwa ni laki tano kwa Simba kutokana na mashabiki wake kuanzisha vurugu kwa askari wakati wa mapumziko na nyota Bernard Morrison amepigwa adhabu ya laki tatu kwa kosa la kinidhamu pamoja na kufungiwa mechi tatu.


8 COMMENTS:

  1. Kwa la nidhamu ya Morrison na adhabu ya kufungiwa mechi tatu inamaanisha Juma Nyosso alionewa au watoa adhabu hawajielewi. Ikiwa Nyosso alimdhalilisha Boko je Morisson hajadhalilisha watazamaji na soka lenyewe?

    ReplyDelete
    Replies
    1. kuna tofauti gani ya kuvaa bukta ya kuchezea mpira na chupi?

      Delete
  2. Zahera alipigwa faini,na kufungiwa kwa kosa la kuvaa kaptula, lakini baadaye sheria hule ikafutika baada ya zahera kuondolewa yanga maana makocha wengine hawakuguswa kwa kosa lile lile. Leo morisoni kavua nukta kabaki na chupi faini laki tatu. Juma Nyosso akafungiwa mwaka mzima. Double standard!

    ReplyDelete
  3. Azabu ya Morrison siyo laki tatu mwandishi soma viziti

    ReplyDelete
  4. Kucheza kwa Morison kutategemea kesi yake, kwahiyo hata TFF wasipo mfungia poa tu, muda utaongea, maana wao sikuzote wako kwaajili ya kuwasaidia mikia fc

    ReplyDelete
  5. Mukoko wa kaonewa kwasababu wananchi walikuwa wameshaanza kuelemewa vibaya na Mnyama na ilikuwa hakuna njia nyengine kuwa nusura kutokana na kipigo cha mapema isipokuwa kumpiga kiwiko Bocco kupunguza kasi ya mikia. Hio ilikua haki yao kuhifadhi heshima yao. Tutaona mengi

    ReplyDelete
  6. Adhabu zote zilizotolewa na sawa ila kwa Mukoko mngemuongeza adhabu naona kama mmembeba ilipaswa apelekwe pia kwa Mwakinyo akajipime huko pia huwenda mpira siyo fani yake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic