NYOTA Mukoko Tonombe kiungo wa Yanga amepigwa faini ya shilingi laki tano kwa kosa la kumpiga
kiwiko mshambuliaji wa Simba, John Bocco kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la
Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Julai 25.
Pia Mukoko amefungiwa mechi tatu kwa kosa hilo ambalo aliliafanya na alionyeshwa kadi nyekundu ya jumlajumla.
Pia taarifa imeeleza kuwa kipa wa Yanga, Farouk Shikalo amepigwa faini ya laki tano kwa kosa la kukwepa kusalimiana na wachezaji wa Simba pamoja na waamuzi jambo ambalo ni kinyume cha kanuni.
Naye Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amepigwa faini ya laki tano
kwa kosa la kugoma kuhudhuria mkutano wa Waandishi wa Habari.
Hii ni kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kutokana na kikao cha Kamati ya Mashindano ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kilichokutana Julai 27.
Pia Simba imepigwa
faini ya shilingi milioni mbili kwa kosa la viongozi na mashabiki kukaidi
maelekezo na kuanzisha vurugu kwa
kulazimisha kuingia mlango usio rasmi na shilingi laki tano kwa kosa la
viongozi kuingia uwanjani kwa mlango usio rasmi.
Adhabu
nyingine ilikuwa ni laki tano kwa Simba kutokana na mashabiki wake kuanzisha
vurugu kwa askari wakati wa mapumziko na nyota Bernard Morrison amepigwa adhabu
ya laki tatu kwa kosa la kinidhamu pamoja na kufungiwa mechi tatu.









Kwa la nidhamu ya Morrison na adhabu ya kufungiwa mechi tatu inamaanisha Juma Nyosso alionewa au watoa adhabu hawajielewi. Ikiwa Nyosso alimdhalilisha Boko je Morisson hajadhalilisha watazamaji na soka lenyewe?
ReplyDeletekuna tofauti gani ya kuvaa bukta ya kuchezea mpira na chupi?
DeleteZahera alipigwa faini,na kufungiwa kwa kosa la kuvaa kaptula, lakini baadaye sheria hule ikafutika baada ya zahera kuondolewa yanga maana makocha wengine hawakuguswa kwa kosa lile lile. Leo morisoni kavua nukta kabaki na chupi faini laki tatu. Juma Nyosso akafungiwa mwaka mzima. Double standard!
ReplyDeleteAcha roho ya kwanini
DeleteAzabu ya Morrison siyo laki tatu mwandishi soma viziti
ReplyDeleteKucheza kwa Morison kutategemea kesi yake, kwahiyo hata TFF wasipo mfungia poa tu, muda utaongea, maana wao sikuzote wako kwaajili ya kuwasaidia mikia fc
ReplyDeleteMukoko wa kaonewa kwasababu wananchi walikuwa wameshaanza kuelemewa vibaya na Mnyama na ilikuwa hakuna njia nyengine kuwa nusura kutokana na kipigo cha mapema isipokuwa kumpiga kiwiko Bocco kupunguza kasi ya mikia. Hio ilikua haki yao kuhifadhi heshima yao. Tutaona mengi
ReplyDeleteAdhabu zote zilizotolewa na sawa ila kwa Mukoko mngemuongeza adhabu naona kama mmembeba ilipaswa apelekwe pia kwa Mwakinyo akajipime huko pia huwenda mpira siyo fani yake
ReplyDelete