BAADA ya Yanga kukamilisha usajili wa aliyekuwa beki wa kulia wa AS Vita, Shaban Djuma, beki wa kulia wa Yanga,Kibwana Shomari ameufungukia usajili huo, huku akimkaribisha ndani ya klabu hiyo.
Kibwana na Djuma wote wanacheza nafasi moja wakiungana na Paul Godfrey, 'Boxer' katika kuwania namba kwenye kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Nasreddine Nabi.
Akizungumza na Spoti Xtra, Kibwana alisema ujio wa Djuma ndani ya Yanga sio suala geni kwenye mpira kwani ili timu iweze kuwa bora basi huhitaji kuwa na wachezaji bora kwa manufaa ya pamoja.
“Suala la Yanga kusajili beki mwingine wa kulia sio geni kwenye mpira, hivyo mtu kutoka sehemu moja kwenda nyingine kama ilivyotokea kwa Djuma ni vitu vya kawaida na mpira ndio ulivyo, hata sisi hatukuwa hapa lakini leo tupo Yanga.
"Ni faida kwa timu yetu kuwa na wachezaji bora ili kuisaidia timu kufanya vizuri, hivyo muhimu ni kutimiza majukumu ambayo mwalimu anatupatia wachezaji kwa ajili ya kufikia malengo yetu, kama ni kweli amesajiliwa na Yanga tunamkaribisha,” alisema beki huyo.
Djuma tayari amesaini dili la miaka miwili kuitumikia Yanga akitokea Klabu ya AS Vita ya Congo ambapo alikuwa ni beki tegemeo kikosi cha kwanza.
UKISEMA YANGA YAFUNGUKIA HALAFU ALOSEMA NI MCEZAJI SIO KICHWA CHA HABARI KIZURI KUTOKANA NA UANDISHI UNAVYOTAKA,KIBWANA SIO MTU WA MENEJIMENT HIVYO KAULI YAKE HUWEZI KUSEMA YANGA IMESEMA UANDISHI UNAENDA KUBAYA SANA
ReplyDelete