July 26, 2021

 BAADA ya kupoteza katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho, uongozi wa Yanga umebainisha kuwa kwa sasa hauna la kufanya.



Ilikuwa jana Julai 25, mwisho wa reli Kigoma ambapo ilichezwa fainali iliyoshuhudia miamba miwili ikimenyana, Simba na Yanga ambao ni watani wa jadi.


Dakika 90 zilikamilika na ubao wa Uwanja wa Lake Tanganyika ukisoma Simba 1-0 Yanga huku mtupiaji akiwa ni Taddeo Lwanga dk 76 kwa kichwa akiwa ndani ya 18 baada ya Luis Miquissone kupiga kona.


Injinia Hersi Said ambaye anatoka katika kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Yanga amesema kuwa kwa kilichotokea hawana cha kufanya.


"Hatuna cha kufanya kwa kuwa imeshatokea na ilikuwa fainali na kila mtu ameona kwamba ilikuwa ngumu na mwisho wa siku tumepoteza hivyo tunajipanga kwa wakati ujao.


"Wachezaji wamejitahidi na wamefanya kazi nzuri hivyo wanastahili pongezi katika hilo. Wakati ujao tutafanya vizuri,".

6 COMMENTS:

  1. Kwa nara ya kwanza kuisikia yanga ikikiri kushindwa bila ya kutaja wameonewa kwasababu tangu mwanzo wa mchezo ilionekana Mnyama kuwa na mkono wa juu na kipundi cha pili unga ukazidi maji na faulo hatari zikatendeka bila ya sababu zozote. Kukiri kushindwa ni uungwana mkubwa na iliobaki kujipanga upya. Ukianguka unyanyuke

    ReplyDelete
  2. Yanga msijali timu yetu ni bora kuliko Simba, wanashinda kwa kubebwa.... Akili za hivi unaweza kuziitaje?? Matusi hayaruhusiwi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mpaka tuwe pungufu ndio washinde. Wanategemea kubebwa mpaka lini? Wameshakuwa virobaaaa

      Delete
  3. Hebu tuwe wakweli jamani na tuache mihemko. Hivi kati ya Yanga na Simba kwa mechi ya jana ni nani alienebwa kama si Yanga?!

    ReplyDelete
  4. Mwaka jana mbona mlikuwa kamili na mkafungwa 4,mnapendaga kulalama sana nyie,na mkienda kimataifa ma timu yenu ya judo mtakuwa mnakula nyingi,timu halichezi soka bali judo na ngumi

    ReplyDelete
  5. Wewe mkia Hilo awali kamuulize dadako pale alikuwepo SASI Mzee wa Penat na huyo Mmanyala sisi tunataka justice Simba Mpira tunawazidi Ila wao wamejipanga kuiba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic