July 26, 2021

 VIVIER Bahati, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa msimu wa 2020/21 ulikuwa na ushindani mkubwa jambo ambalo linawapa somo la kujipanga kwa wakati ujao.



Azam FC ilikuwa na malengo makubwa matatu, kutwaa taji la ligi, taji la Kombe la Shirikisho pamoja na kumaliza ndani ya nafasi mbili za mwanzo.


Yote yamekwama kwa msimu wa 2020/21 kwa kuwa katika Kombe la Shirikisho waliishia hatua ya nusu fainali kwenye ligi wamemaliza nafasi ya tatu vinara ni Simba na nafasi ya pili ipo mikononi mwa Yanga.


Bahati amesema:"Haukuwa msimu mzuri kwetu ila vijana walipambana katika kutimiza majukumu yao hilo kwetu ni jambo la msingi na tunajivunia.


"Kwa wakati ujao imani yetu ni kuona kwamba tunafanya vizuri zaidi na kufikia malengo ambayo tunayahitaji hivyo mashabiki watupe sapoti," amesema. 


Ni pointi zao 68 kibindoni baada ya kucheza mechi 32 namba moja ana pointi 83 ambaye ni Simba na namba Yanga pointi 74.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic