August 4, 2021

 HAJI Manara aliyekuwa Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa Mtendaji Mkuu wa zamani wa Simba,  Senzo Mbatha aliajiliwa ili aweze kumfukuza kazi.


Haji alibwaga manyanga ndani ya Simba kupitia kundi la Simba HQ baada ya kutokuwa na maelewano mazuri na mabosi wa Simba.



Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari leo Manara amesema kuwa alipoletwa Mbatha kutoka Afrika Kusini aliniita ofisini na kuniambia kwamba waajiri wamemuambia kazi yake ya kwanza ni kumfukiza yeye.


"Senzo aliniita ofisini akaniambia kwamba kazi ya kwanza ambayo amepewa na mabosi waliomuajiri ni kumfukuza kazi yeye jambo ambalo yeye alilikataa.


Mbatha aliniambia kwamba hakuona maana ya kunifukuza kwa kuwa alikuwa hajafanya nami kazi na aliona ile Simba day ya 2019 hivyo ni mtu muhimu. 


"Nilibaki Simba ila kwa kuwa ilikuwa hivyo nikafanya naye kazi kwa ushirikiano na kila kitu kiliendelea mpaka pale ambapo Senzo akaondoka nikajua kwamba anayefuata ni mimi," amesema Haji Manara.

13 COMMENTS:

  1. Hiyu aache ujinga wake. Ameshaondoka simba basi ae de kwa amani asianze kurudi rudi kuanzisha zogo hakuna atakae muelewa tena. Kwanza kama kila mtu akitaka kueleza mambo yake ataita press nchi hii itakuwa vipi. Haji hana tena platform ya kuzungumza alikuwa anatumia ya simba.

    ReplyDelete
    Replies
    1. KHAJI MANARA ameongea maneno mengi ila ndio amezidi kuharibu au kujiharibia zaidi kwenye proffesional yake.
      Zingangatia Mambo haya kadhaa kama kichwa chako kinafanya kazi vizuri basi utagundua KHAJI MANARA ana matatizo tena makubwa.

      (1) Waswahili wanasema usiwatukane wakunga yaani wasaidizi wanaomsaidia mjazito kuzaa wakati bado uzazi ungalipo. KHAJI kaamua kuivua nguo Simba hadharani katika Mambo yaliyofanyika ndani ya taasisi. Khaji katika mawazo yake haoni kuwa ipo siku anaweza kurudi tena Simba na kuomba ajira ndani ya Simba? Na si Simba tu,ni taasisi gani makini Tanzania itakayokuwa na hamu kufanya kazi na khaji Manara Kama anasema Simba imo kwenye Damu yake halafu anatoka hadharani na kuivua nguo na masimango kadhaa vile alikuwa kaekewa kisu Cha Roho lazima aitumikie Simba?
      Vipi taasisi ambayo khaji hana mapenzi nayo itakuwaje ikija ikitokea sinto fahamu?
      Unapozumzia suala la mapenzi na kitu fulani sio kitu cha mchezo mchezo Bora hata kupoteza maisha kuliko kuona unachokipenda kinanyanyasika seuze leo mwenye mapenzi mwenyewe ndie anaenyanyasa like anachokiopenda itakuwa ni mapenzi hayo au unafiki?
      (2) Kama Kahaji Manara analalamika kujitokeza Simba,Mwinyi Zahera Mkongomani haijui Yanga hata ilipotokea lakini aliibeba Yanga kwenye mgongo wake akitumika muda,nguzu na pesa zake binafsi kuhakikisha Yanga wanavuka Kwenye kipindi kigumu. Kwa bahati mbaya Zahera kafukuzwa Yanga bado akiwa anaidai Yanga lakini hatujamuona Zahera akiitisha preconference kuikashufu Yanga sisi ni watu wa hovyo.
      (2) Huwezi kushinikiza kutoa tuhuma za upande mmoja ili kuwaaminisha watu kuwa upo sahihi kwa yale unayoyasema. Kanuni za mtu binafsi ambae anafanya kazi taasisi ambayo anahisi hatendewi haki ni kuacha kazi simple, tena kuacha kazi kwa amani sio kwa matusi kwani uliamua kufanya kazi kwa hiari yako kwa kujitolea huna mkataba nothing vipi iendelee kuteseka? leo unakuja mbele za watu kujalalamika kuwa umeonewa na bahati nzuri zaidi Manara alishakuja hadharani Mara kadhaa kusema kuwa Simba sio wazee wake kilichokuwa kinamueka Simba ni kitu gani?
      (3) Uadui wa Khaji kwa Barbara unachangiwa zaidi na urafiki wa karibu kati ya Senzo na Khaji. Senzo yupo very tactical minded person ni Rahisi tu kwake kumburuza Manara kwenye conflict ama mgogoro kati yake na Barbara lengo kubwa la Senzo ni kutaka kuona Barbara anafeli ndani ya simba na kwa maelezo ya khaji angefurahi kuona Senzo anaendelea kushikikilia nafasi ya CEO. SENZO alijua kabisa kuwa karibu na Manara ni kuwa karibu na wanasimba ila kwa bahati mbaya huwezi kumtakia mabaya Barbara bila kuizuru simba.
      (4) Barbara anatakiwa kuwa mvumilivu achape kazi. Hatuwezi kusema kuwa Barbara ni malaika hana Makosa, kila binaadamu ana mapungufu ila Barbara ameingilia shughuli ambazo zimegubikwa na mfumo dume na si ajabu moja ya umarufu wa Simba hivi sasa Duniani ni huu uamuzi wa Simba kuendeshwa na CEO Mwanamama. Vyombo vya habari vya ndani, Marekani na Ulaya viliripoti kwa mashangao kiasi, kama vile vilikuwa haviamini kinachoendelea kutokana na wadhifa huo wa Barbara nadhani walishangazwa Jambo hili kutokea Africa.
      Sasa Kampeni za kufa mtu za Khaji Manara na Senzo kuhakikisha Barbara anang'oka kwenye nafasi yake ya kazi,wazungu hawakuwa wajinga kushangazwa kuona mwanama ni Msimamizi mkuu wa moja ya klabu kubwa barani Africa.
      (5) Wanasimba wanatakiwa kutulia hasa kipindi hiki ambacho mara nyingi ni kipindi Cha furaha kutokana na heka heka za usajili lakini Manara anatumika kuwapotezea hamasa wanasimba zidi ya timu yao lazima wawe nae makini kwani Iblisi ni miongoni malaika waliomghasi Mungu lakini inasemekana asili ya Iblisi ni miongoni mwa malaika mwenye DNA ya ushetani kwa hivyo hata alipokuja kukengeuka kuja kumughasi Mungu ilikuwa ni kitu kuja
      kuthibitisha uasili wake.☹️

      Delete
  2. Aache ujinga hatutaki uppuzi wake tena

    ReplyDelete
  3. Nenda huko kawape siri Yanga. Unatakiwa uwe na akili na uwe na heshima kwa maboss wako unamuona mwenzako NUGAS Jifunze kutoka kwake Pumbavu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli mikia leo wanamtukana Manara? SIAMINI. Au ni vibaraka wa mtu fulani nini?

      Delete
  4. Pole sana Manara. Nenda kafufue Simba SC (original ) yenye Makao yake pale Msimbazi. Ona baadhi ya mashabiki vibaraka wa Simba wanakusaliti leo.SSC imetekwa na ni ya Familia moja kwa sasa. Kila kitu ni mali yake. Baada ya kuona umeifikisha SSC mahali ilipo wameamua kukufukuza.kweli binadamu hawana wema.

    ReplyDelete
  5. Simba haina tabia ya maneno ya chokochoko, kila kitu kinakwenda kwa mipango. Hata pale inaponyinwa penelti ya haki, sio kama wengineo kupiga makele na kupenda kufunguwa makedi ba badala yake husahau na kuishughulikia timu kwa maendeleo take. Hawana muda wa kushutumiana au kuzozana baina ta mashabikib na viongozib bali kuweka maslahi ya timu kwanza na hayo ndio siri ya mafanikio

    ReplyDelete
  6. Manara ana haki ya kulalamika, anefanya juhudi kubwa sana kufikisha Simba ilipo, baadhi ya watu wanaangalia upande ulio na pesa ndio maana hawampithamani tena

    ReplyDelete
  7. Mbona yeye alipokuwa ana mic anamshangilia mo. Leo anamkashifu. Hi timu si yake alifanya kazi ya kuhamasisha alivyo ajiriwa. Asiseme kuwa alikuwa anahamasisha bure

    ReplyDelete
  8. Kusema kweli Haji kakosa hekima na hana hata washauri! Haji angekumbushwa ule usemi wa "jogoo mwenye hekima huchagua wakati wa kuwika"
    Kwa tabia na hulka zake, hata mimi ningekuwa CEO wa Simba, mingemfukuza Haji siku nyingi.
    Wala hapa Haji asijifanye rafiki wa Senzo, alipoondoka Simba; Haji alikuwa mtu wa kwanza kumsakama Senzo, kwa maneno makali sana. Sasa anamtega uswahiba?
    Hayo anayoyasema sasa angeyasema zamani tungemuelewa; siyo sasa!
    Masuala ya kimkataba ni masuala binafsi sana, ni sawa mke mkishatalikiana ajitokeze kudai "mme gani kwanza ana kibamia" wenye hekima watapuuza tu!
    Haji nyamaza, Simba mpuuzeni, maisha yaendelee.

    ReplyDelete
  9. Haji, Haji Haji! Tafadhali sana nakuomba utulizane. Hiki unachokifanya kinakuondolea credits. Umeamua mwenyewe kuondoka Simba sasa maneno yote hayo ya nini Bwana Mdogo?!!

    ReplyDelete
  10. leo hii mikia inamtukana Manaraa!hahahahah kwisha habari yenuu aiseeee

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic