LEO Agosti 8,2021 aliyekuwa Ofisa Habari wa Simba Haji Manara ataogea na aandishi wa Habari pamoja na jamii kiujumla kwa lengo la kuwashukuru Wanasimba.
Manara alibwaga manyanga ndani ya Simba baada ya kufanya kazi kwa mafanikio makubwa na sababu kubwa ya yeye kubwaga manyanga haikuwekwa wazi na mabosi wa Simba.
Kupitia katika Ukurasa rasmi wa Instagram wa Haji Manara ameandika:"Kupitia Wanahabari leo tarehe 4/8/2021 saa tano asubuhi nitaongea na kuwashukuru Watanzania na Wanasimba kwa kunipa nafasi ya kuwatumikia mabingwa wa nchi.
"Heshima mliyonipa nnao wajibu wa kuwashukuru na kusema asante kwenu,ninao pia wajibu wa kushukuru taasisi nyingine zote tulizofanya kazi pamoja.
"Mkutano huu utarushwa live na page hii, (Haji Manara) Manara Tv na Azam Tv,".
Ilikuwa ni Julai 28 taarifa ya kusepa Simba ilipotolewa na mbadala wake aliyetangazwa ni Ezekiel Kamwaga.
Huyu ameshindwa nini kukaa kimya si kapata alichokuwa anakitafuta? Wakati mwingine ni kutaka kuleta fujo tuu, watu wameshafuta habari zake aendelee na maisha ayapendayo. Hii inaonyesha bqdo haamini kama sasa yuko nje ya simba. Na bqdo qtakoma sana, hakujua kuwa alikuwa maarufu kwa mgongo wa simba na sio hao waliokuwa wanamtumia gizani. Ajipange maisha ndio kwanza yanaendelea.
ReplyDeleteAnahaki ya kuzungumza nadhani kahaji Kama angekuwa ana meneja au Mwanasheria wa kumsimamia shughuli zake asingeropoka maneno yale zidi ya Bosi wake. Yote kwa yote KHAJI alifanya kazi vizuri ndani ya simba Ila alieka urafiki mbele kuliko ajira yake aliokuwa anaitumikia kwa nguvu tu.Ulimi ukiweza kuutumia vizuri ni utajiri lakini kama huna uhakika na matumizi ya ulimi wako basi bora ukae kimya la sivyo ufakiri utakuhusu.
DeleteSisi simba tulishamalizana nae, atulie tuu. Kuaga gani anakotaka kama sio kuanzisha choko choko
ReplyDeleteMuachini naenataka kurudi mjini, kivingine
ReplyDeleteDah! jamaa mpaka anatia huruma, mjini kuna mambo sana
ReplyDeleteKuacha kazi ni rahisi kuupata kazi mpya ni ngumu
ReplyDeleteSi uongo
DeleteAliyoyasema Manara hayana uzito wa kuyaongelea katika press comfrence
ReplyDelete