BREAKING: KAZI inaendelea ndani ya kikosi cha Azam FC ambapo leo Agosti 3 ametambulishwa mchezaji mwingine ambaye ni kipa.
Kupitia ukurasa rasmi wa Azam FC wameandika namna hii:-Azam FC tunayofuraha kuwataarifu kuwa tumeingia mkataba wa miaka miwili na golikipa, Ahmed Ali Suleiman 'Salula', tuliyemsajili kutoka KMKM ya Zanzibar.
Golikipa huyo mwenye umbo kubwa, amesaini mkataba huo mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat'.
Salula ni mmoja wa makipa hodari, akiwa ndio tegemeo katika timu ya Taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes', anakuja kuongeza nguvu katika eneo la langoni kwenye timu yetu.
Huo unakuwa usajili wetu wa saba kuelekea msimu ujao, tukiwa na nia ya dhati ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CC).
Wachezaji wengine tuliowasajili ni beki wa kushoto, Edward Manyama, kiungo mkabaji, Paul Katema (Zambia), viungo washambuliaji, Charles Zulu (Zambia), Kenneth Muguna (Kenya) na washambuliaji Rodgers Kola (Zambia), Idris Mbombo (DRC).
Karibu sana Azam FC, Salula
0 COMMENTS:
Post a Comment