August 3, 2021



 

KLABU ya Simba imempa mkataba wa miaka mitatu winga wa kimataifa wa Malawi, Peter Banda ambaye alikuwa anakipiga  kwa mkopo ndani ya Klabu ya Sheriff ya Moldovia.

Winga huyo anahusishwa amekuja Simba kwa ajili ya kuziba nafasi ya Luis Miquissone anayetajwa kuingia anga za Al Ahly ya Misri.

Nyota huyo alikuwa ni mchezaji wa Big Bullets ya Malawi na jana alivuruga mambo kwa kile ambacho kilielezwa kuwa amepewa dili na mabosi wa Yanga.

Leo Simba wamemtambulisha rasmi kwenye ukurasa wa Instagram kwa kuandika kwamba 'Peter Banda ni Simba'.

19 COMMENTS:

  1. Mseme tu mlikuwa mnawatekenya utopolo, au wamemsajili Peter msechu

    ReplyDelete
  2. Utopolo wanakata rufaa Cas kanuni hazikufatwa hapo

    ReplyDelete
  3. Ila yanga wana mambo ya kishamba sana. Sasa kuwadanganya mashabiki wao itawasaidia nini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Upo sahihi kabisa kiongozi...ila ktk hili tusisahau ujinga huu kwa kiasi kikubwa sana huwa unachangiwa na waandishi wa habari fulani fulani hivi, ambao sina hakika kama kweli wamesomea journalism. wengi ni wavivu sana wa kufanya research (japo kdg) ya story wanayoiandika.

      Delete
  4. Yanga hawawezi kupigania vita ya mchezaji anaetakiwa na Simba halafu Yanga ashinde vita. Ukiona mchezaji kaenda Yanga basi ujue simba hawajamuhitaji.
    Ninachowaasa Simba chonde chonde.
    (1) Kwakuwa nafasi za kuongeza Wachezaji wa kigeni ni finyu basi wasidharau vipaji vya ndani hata kidogo.
    (2)Tadeo Lwanga Anahitaji pacha mwenye uwezo Kama yeye au kuzidi katika eneo la kiungo.
    (3) Kama utaniuliza Kati ya Kagere na Mundele Mukusu basi bila ya kupepesa Macho Mundele yupo Bora zaidi kuliko Kagere.Mukusu ni mpambanaji,Ball holding forward,defending and scorer. Wakati mwengine hii hofu ya kusema sijui tukimuacha mchezaji fulani atakwenda timu fulani umepitwa na wakatii tufokasi Zaidi kunako ubora wa mchezaji,kagere kwa sasa ndani ya simba hatoi kile kinachohitajika kwenye mahitaji makuu ya timu.
    (4) Beki wa Kati Kama atapatikana Mzawa wa kwenda kuwatia purukashani akina Onyango basi ni suala la kulifanyia kazi haraka. Akina Kenedi juma Kama wanawaogopa akina Wawa,wanawaheshimu sana badala ya kustep up na kumfanya Gomezi ajiulize nani wa kumpanga.
    (5) Simba wasivimbe kichwa wakifikiri Wana timu nzuri Sana Africa. Maboresho ni lazima tena ya kiufundi zaidi katika kutafuta wachezaji wa maboresho ili kikosi kije kuendena na mahitaji halisi ya malengo timu iliyojiekea. Tunajua Simba Kuna watu makini kwenye masuala ya usajili ila ikiwa Alahly Mabingwa watetezi wa klabu bingwa Africa wanahaha kukiongezea nguvu kikosi Chao. Sasa kama Simba wataridhika na timu waliokuwa nao Sasa kuwa inatosha basi utakuwa mdhaha huo sio serious.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Swadkta kwa hoja zako ulizotoa na nakubaliana kwa asilimia 100 kuwa ni muda muafaka kuachana na Meddie Kagere hata akiamua kwenda timu pinzani maana sioni anacho deliver kwenye timu hasa ukizingatia ni mchezaji ambae mfumo wa makocha Sven na Gomes unaonekana sio rafiki kwake.Nakubaliana kusajili mshambuliaji mwenye kuhold mpira, spidi na mwenye target na goli kama Mundele Mukusu.
      Kiungo mkabaji Jonas Mkude, ni bora wakamuacha aende anakoona anaweza kupata furaha zaidi ya Simba na kutaka kusujudiwa kama mtoto wa mfalme.Kuna viungo wengi sana na wa uhakika ambao wamepita klabu ya Simba na hakuwa na atitude hii ya Jonas na mfano mdogo kina Khalid Abeid, Aluu Ali, Nico Njohole, Omari Gumbo n.k.
      Namkubali Kennedy Juma kuwa ni mchezaji mwenye kutumia akili na nguvu lkn inabidi aongeze bidii na awe serious ili kumuondoa Wawa ambaye anaonekana kuchoka hasa ukizingatia msimu ujao mechi zitakuwa nyingi na atakiwa kuwa na mbadala wa uhakika.
      Nakubaliana sana na hoja yako No.5-Simba wasivimbe kichwa wakifikiri Wana timu nzuri Sana Africa. Maboresho ni lazima tena ya kiufundi zaidi katika kutafuta wachezaji wa maboresho ili kikosi kije kuendena na mahitaji halisi ya malengo timu iliyojiekea. Tunajua Simba Kuna watu makini kwenye masuala ya usajili ila ikiwa Alahly Mabingwa watetezi wa klabu bingwa Africa wanahaha kukiongezea nguvu kikosi Chao. Sasa kama Simba wataridhika na timu waliokuwa nao Sasa kuwa inatosha basi utakuwa mdhaha huo sio serious.

      Delete
  5. Nyie wote ni wapuuzi tu, hakuna kiongozi yeyote wa yanga au taarifa rasmi toka kwenye vyanzo vya klabu viliyisema yanga imemsajili uyo mchezaji zaidi ya tetesi za kwenye mitandao, sasa waandishi mnatunga jambo wenyewe na mnalikanusha wenyewe, acheni utahaila,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Maneno ya madalali wao wanasema Yanga ili wawapige kwenye dili kama kawaida.. hehehe

      Delete
    2. Hakuna cha madalali wala nini hao ni wanahabari tu wanauza habari zao ila pia ukweli ni kwamba Utopolo hawawezi kugombania mchezaji na Simba halafu wakashinda kwa sasa

      Delete
  6. Nilitaka kushangaa, yanga wamsajili hiyo dogo? Angekuwa anatoka congo na hasa vita club hilo ningeamini

    ReplyDelete
  7. Nyasa Big Bullets winger Peter Banda has signed a three-year deal with Simba Sport Club of Tanzania after the two clubs reached an agreement over his sale on Tuesday.

    The transfer has been confirmed by Bullets Chief Executive Officer Suzgo Nyirenda.



    “It is my great pleasure to announce the transfer of our player Peter Banda to Simba Sports Club of Tanzania. Peter will sign a three-year deal with Simba and Nyasa Big Bullets FC will get 8% of and future transfer of the player to any club.”

    “We would like to thank Simba SC for the good and cordial negotiations and we would like to thank Peter for being a wonderful player to us during a period in which he won player of the year in Malawi in 2019,” said Nyirenda.

    His move follows the expiry of his loan deal at FC Sherriff Tiraspol of Moldova on 31st July, 2021.

    Banda joined FC Sheriff on a six-month loan deal from Bullets in February with an exclusive option to buy.

    However, the Moldovan side did not activate the clause for the Malawi international’s permanent transfer.

    He scored 7 goals and provided 10 assists during his stay at FC Sheriff. His last involvement with the Moldova champions was on July 28 in the UEFA Champions League group stages against Alashkert of Armenia.

    Banda joined Bullets from Griffin Youngsters and played for a season in which he helped The People’s Team defend the TNM Super League championship.

    Apart from Simba SC, rivals Young Africans were also interested in the services of the player but failed to win the race as he set his eyes on playing for the Tanzanian champions.

    He is likely to fly out to South Africa for Simba SC’s pre-season training

    ReplyDelete
  8. Simba raha ikamilike pga chini Kagere na Mugalu leta Okwi na Fraga nafasi ya Chikwende apewe Banda apo mchezo umekamilika.

    ReplyDelete
  9. Mimi sikubaluani na wadau wenzangu wa Simba waliotoa maoni kuhusu Kagere,ukiangalia takwimu za Kagere zinatisha Bila kuweka figisu anamzidi Bocco,misimu miwili top scorer,champion league 2018 seven goals,msimu huu pamoja na kucheza match chache magoli 13,huu ni usanii uliotengenezwa na viongozi wenye chuki na Matola ili tuamini Kagere ameshuka kiwango kitu ambacho c kweli.Haya yalimkuta Hamis Tambwe msimu wa 2013 alikuwa mfungaji bora VPL viongozi wakasema ameshuka kiwango,akaenda Young akawa mfungaji bora mara mbili.Figisu hizi za kipuuzi zishapitwa na wakati kwa sababu Mess na Ronaldo cyo waspaniola lakini hawajawahi kufanyiwa figisu Spain.Haya ndiyo yaliyomkuta Chikwende,amecheza match Saba tu tangu asajiliwe akafunga magoli manne,tunaambiwa Hana kiwango na waandishi wapuuzi wanatuamunisha lakini one day the truth shall prevail.Mpira wa Kibongo viongozi wasipoacha ujanja ujanja wa kupiga deal za usajili mpira wetu hautakua kamwe.Tujifunze Tp Mazembe,ilipochukua ubingwa mara mbili mfululizo Africa ilikuwa na Wazambia 8 lakini hawakufanyiwa figisu za kipuuzi kwani sisi tunachongalia ni matokeo ya Club na c ubaguzi wa Taifa mtu analotoka.Bora Luis Miqssuine ameondoka kwani naye yangemkuta.Mfalme Chama naye bora aondoke Sasa hivi,kwani huko mbeleni naye ataanza kuwekwa bench na tutaanza kuaminishwa kwamba Clatous Chama ameshuka kiwango kwa kutumia waandishi uchwara.Sasa nimeamini maneno aliyosema Mwinyi Zahera kwamba mchezaji was nje anayejitambua vema hawezi kuja kucheza Tanzania,kwani chuki na figisu za viongozi ni mbaya mno na ndiyo maana mpira wetu haukui.Kweli mpira wa Bongo kichefuchefu.Waandishi na wadau tusaidieni kufichua madudu haya.

    ReplyDelete
  10. Hakuna chuki Wala nini, Kagere mchezaji mbaya ila haiwezekani makocha wawili Bora wenye falsa tofauti waone wangetamani kuwa na straika mwenye uwezo zaidi ya kagere halafu tuseme Kagere anaonewa. Licha Mugalu kutokuwa na utulivu uliokamilika katika kupasia nyavu lakini Kagere bado akashindwa kumueka benchi.Simba licha ya kutoa mfungaji Bora kwa sababu tu ya akina prince Dube kusumbuliwa na majeraha na Yanga kukosa washambuliaji la sivyo hata ubingwa Simba ungekuwa mashakani.

    ReplyDelete
  11. Watu hawanakumbukumbu mbona Simba walimtaha Djuma Shaban wakazidiwa na Yanga, acheniushabiki wa kishamba

    ReplyDelete
  12. Simba walimtaka Mwamnyeto lkn Yanga ikawazidi kete, mashabiki wa mikia fc acheni kuaminishwa upuuzi mkabeba kama hamjielewi

    ReplyDelete
  13. Na huko hana jinna lolote, ni huko Simba angelikuwa zamani ananyanganyiwa kimataifa kama ilivo kwa Konde Boy, Manula, Onyango, Chama, Shabalala ns wengineo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic