BREAKING: DILI la usajili wa mshambuliaji wa zamani wa Horoya AC ya Guinea, Heritier Makambo limekamilika ambapo leo ametabulishwa rasmi ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.
Makambo ni kati ya wachezaji waliokuwa kwenye mipango ya kusajiliwa na Yanga katika usajili wa msimu huu katika kuisuka safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
Nyota huyo anaijua sera ya Yanga kwa kuwa alisepa hapo msimu wa 2018/2019.
Mshambuliaji huyo amepewa dili la miaka miwili ndani ya Yanga.
Makambo alitua Bongo Juzi kwa ajili ya kumalizana na mabosi wa Yanga na baada ya kukamilisha utaratibu wa mwisho amesaini ndani ya timu hiyo ambayo inajiimarisha kwa ajili ya msimu ujao na itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ndio hili jambo la leo la wananchi? Tomu inaongozwa kiswahili swahili tuu
ReplyDeleteYanga kumsajili makambo ni sawa na simba kumsajili okwi, hawana jipya hao.
ReplyDeleteOkwi atacheza FDL lkn Makambo atacheza Premier League hiyo ndio tofauti tarehe 24 haiko mbali CAS hoyeee
DeleteHaya poa
ReplyDelete