KUNA hatihati nyota wa Simba mzawa Miaraj Athuman, 'Sheva' msimu ujao asiwepo ndani ya kikosi hicho kutokana na mabosi wa Namungo kutwaja kuwania saini yake.
Sheva hakuwa na msimu bora kwa 2020/21 licha ya timu yake kutwaa taji la Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho pamoja na taji la Ngao ya Jamii.
Aliweza kurudi kwenye ubora wake kupitia mashindano ya Mapinduzi ila ghafla kasi yake iliyeyuka baada ya kupata majeraha.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimelifikia gazeti la Spoti Xtra zimeeleza kuwa nyota huyo anaweza kuachwa baada ya kandarasi yake ya miaka miwili kuisha.
"Upo uwezekano wa Sheva kuachwa ndani ya Simba kutokana na ushindani wa namba pamoja na kuhitajika na timu nyingine.
"Ni suala la kusubiri kuona itakuaje kwani ripoti ya mwalimu, (Didier Gomes) imeeleza wachezaji ambao watatakiwa kuachwa," ilieleza taarifa hiyo.
Msimu wa 2019/20 nyota huyo alikuwa kwenye ubora wake na alifunga mabao 7 licha ya kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.
Alijiunga na Simba akitokea Lipuli ya Iringa ilikuwa ni msimu wa 2019/20 ambapo alisaini dili la miaka miwili.
Aende Yanga
ReplyDeleteYanga wanasema hawawataki wachezaji wa Simba kwasabsbu hawana kiawango cha kuichezea timu yao
ReplyDeleteHuyo naye Mchezaji Ni Kama yule Mo Ibrahim,Ndemla nk wote size yao KAGERA,MTIBWA nk
ReplyDelete