August 6, 2021


 KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama, amefunguka kuwa atamsapoti mchezaji mwenzake na rafiki yake mkubwa, Luis Miquissone ikiwa nyota huyo atafanya maamuzi ya kukubaliana na ofa 
ya kujiunga na Mabingwa wa Afrika, Al Ahly.


Al Ahly 
wamekuwa wakiiwinda saini ya Luis kwa muda mrefu sasa kufuatia mapendekezo ya kocha mkuu wa kikosi hicho, Pitso Mosimane, na hivi karibuni imeripotiwa kuwa wapo tayari kuwasilisha ofa ya dola 900,000 sawa na shilingi bilioni 2 za Kitanzania ili kufanikisha dili hilo.

 

Mosimane amewahi kumfundisha Luis katika Klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, kabla ya Luis kujiunga na Simba huku Mosimane akitimkia Misri.


Luis msimu huu amekuwa katika kiwango kikubwa akifanikiwa kuhusika kwenye mabao 19 kwenye Ligi Kuu Bara pekee, ambapo alifunga mabao tisa na kuasisti mabao 10.


Akizungumza kuhusiana na dili hilo, Chama alisema:

“Kuhusiana na suala la Luis kujiunga na Al Ahly, nadhani hilo ni juu yake kuchagua kama ataondoka, au atasalia Simba, ni kweli Luis ni rafiki yangu, hivyo nitamshauri aangalie sehemu anayoona kwake inamfaa.

 

“Kama akiamua kuondoka nitamuunga mkono, na kama akitaka kubaki nitamuunga mkono pia, hivyo tumuachie yeye na uongozi ufanye maamuzi.”

4 COMMENTS:

  1. Chama kama kweli jembe lako mshauri abaki simba mashabiki bado tunamuhitaji hatuna uhakika kama tutampata mbadala kwa halaka

    ReplyDelete
  2. ss kama washabiki wa simba bado tunamuhitaji sana Luis ila maamuzi yoyote yatakayotolewa na uongozi tunawaunga mkono

    ReplyDelete
  3. Maamuzi yoyote kwetu Wana Simba in sahihi,long live Simba sports club

    ReplyDelete
  4. Chama achana Na mambo ya kubishana Na wajiga wajiga wewe pigs Kazi🔥👍

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic