August 1, 2021

 


KAMATI ya Mashindano ya TFF, katika kikao chake cha Julai 27, mwaka huu kilipitia taarifa ya mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho wa ASFC wa Julai 25, 2021 kati ya Simba dhidi ya Yanga, uliochezwa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma na kujiridhisha kwa majibu wa kanuni, na kutoa adhabu zifuatazo;

Simba

      i.            Klabu ya Simba imetozwa faini ya Shilingi Milioni 2, kwa kosa la viongozi na Mashabiki kukaidi maelekezo, kulazimisha kuingia uwanjani na kupita kwa nguvu kupitia mlango usio rasmi wakati wa kukagua uwanja, na kusababisha uharibifu.

   ii.            Simba imetozwa faini ya Shilingi 500,000 kwa kosa la viongozi kuingia uwanjani, kwa kutumia mlango usio rasmi.

iii.            Simba imetozwa faini ya Shilingi 500,000 kwa mashabiki wake kujihusisha na utovu wa nidhamu.

iv.            Klabu ya Simba, pamoja na viongozi husika wamepewa onyo kali, kwa kukaidi maelekezo, na kuingilia shughuli za utoaji medali na zawadi kwa washindi.

   v.            Mchezaji wa Simba, Bernard Morrison amefungiwa mechi tatu, na kupigwa faini ya Shilingi Milioni tatu kwa kufanya kosa la kinidhamu na udhalilishaji.


Yanga

      i.            Klabu ya Yanga imetozwa faini ya Shilingi Milioni 1, kwa kosa la kutumia mlango usio rasmi kuingia uwanjani.

   ii.            Watendaji na mashabiki wa Yanga walijihusisha na utovu wa nidhamu kwa mwamuzi wa akiba wa mchezo, hivyo wametozwa faini ya Shilingi 500,000.

iii.            Viongozi wa Yanga waliingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi, hivyo wametozwa faini ya Shilingi 500,000.

iv.            Mashabiki wa Yanga waliwashambulia waamuzi kwa chupa za maji wakati wa mchezo, na kutozwa faini ya Shilingi 500,000.

   v.            Viongozi na Mashabiki wa Yanga walilazimisha kupitia mlango usio rasmi kuingia uwanjani wakati wa kukagua uwanja, na hivyo kutozwa faini ya Shilingi Milioni 2.

vi.            Mukoko Tonombe alifanya kosa la kumpiga, John Bocco hivyo kufungiwa mechi tatu pamoja na faini ya Shilingi 500,000.

vii.            Faroukh Shikalo kwa makusudi aligoma kusalimiana na wachezaji wa Simba, na mwamuzi wa mchezo hivyo kutozwa Shilingi 500,000.

viii.            Kocha wa Yanga aligoma kuhudhuria mkutano wa maandalizi ya mchezo na waandishi wa habari, hivyo ametozwa faini ya Shilingi 500,000.

1 COMMENTS:

  1. Na huyu Shikalo ndio aambiwe nini. Ndio ansonesha chuki. kwa Simba ambapo yeye mwenyewe hajijuu kama atabski su kutimuliwa. Kwa matopolo kuna vioja vya kila aina

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic