August 9, 2021


UONGOZI wa Yanga umebainisha kwamba sio Tuisila Kisinda ambaye amepewa ofa bali wapo wengine wengi ndani ya kikosi hicho ambao wamepewa ofa kwa ajili ya kujiunga na timu nyingine.

Injinia Hersi Said, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ndani ya Yanga amesema kuwa suala la kuuza wachezaji wenye hadhi kwa Yanga limekuwa likifanyika.

Hersi ameweka wazi kwamba hilo linatokana na uwezo wa wachezaji ambao wapo ndani ya timu hiyo.

"Suala la kuuza wachezaji limefanyika sana kwa hiyo ofa zipo za wachezaji sio Kisinda tu zipo ofa nyingi kwa wachezaji.

"Kuna ofa ya Yacouba, (Songne), Tonombe, (Mukoko) hivyo ambacho kinaangaliwa ni namna ya kuweza kufanya biashara pamoja na kupata mbadala wake," amesema.

10 COMMENTS:

  1. Hata Sarpong ana Offa pia.Shikalo vile vile.
    Sasa Yanga hata timu hawana wala hawaja accomplish chochote kile Cha maana eti tayari nao wanajigamba kuwa wana ofa?
    Waswahili wanasema usilazimishe Kondoo kunya boga Kama tembo utamsababishia Kondoo maumivu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ahhhh. We hujui huyu ni injinia bweha? Kwa kiwango gani? Wameonekana wapi. Yeye injinia amekuwa na kundi lake la vunga masters senzo na manara na yeye. Hapo hupatikana utatu mdanganyifu

      Delete
    2. Kwani lini walicheza mechi za mana hata ubora wao ukaonekana na kunyanganyiwa na timu tajiri? Ni wachezaji wa Simba waliojiuza baada ya kuonekana ubora wwao. Hapa tusidanganyane ni wivu tu. Wachezaji wa Simba, sio viongozi walionadi kuwa wachezaji wao wanatakiwwa ni timu tajiri ambapo timu hizo zenyewe ndizo zilizotangaza nia kuwataka wachezaji wa ns kukaririwa na magazeti ya nje na ya ndani pamoja na maajenti

      Delete
  2. Mikia acheni kelele, hayawahusu. Angalieni zaidi mambo ya timu yenu na usajili wenu. Yanga tuachieni Wananchi.

    ReplyDelete
  3. Nakumbuka Sapong tuliambiwa ana ofa kutoka klabu 1 China sijui imeishia wapi

    ReplyDelete
  4. Wachezaji wa Simba walipotakiwa, walitajwa wazi matajiri waliowataka na Kama ii kweli wachezaji hao wa yanga walitakiwa kama wale a Simba, vilevile watajeni wazi matajiri waliowataka na kama si hivo mna ogopa kusutws

    ReplyDelete
  5. Tatizo hapa Ni Elimu kwani kuonekana mpaka Mchezaji acheze Club Bingwa?vijana mnatia haibu comment zenu eti walicheza wapi mechi za ushindani hata kamasi zimewaisha ,mbona mnasema Ligi ya Tanzania ni ya nane kwa ubora Africa je ilijulikanaje nashangaa Mwanaume anakuwa na uchungu Kama wakuzaa.

    ReplyDelete
  6. Eti walicheza mechi gani za kiushindani ,inaonekana mna uwezo mdogo wa kufikiri.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic