JAMAA anahitaji ushauri baada ya kuvurugwa na mke wake
Jina langu ni Rwakatare mkazi wa Mwanza pia mke wangu anaitwa Juriana mwenye umri wa miaka 27. MwenyeziMungu katujalia tuna mtoto mmoja wa kike.Mwaka 2018 nirimfungulia mke wangu duka la kuuza nguo za kiume na kike.
Mke wangu alifanya kazi kwa bidii kubwa sana hadi duka letu likapanuka sana japo mimi nilizidi kufanya kazi yangu ya kusafirisha maharagwe kutoka Mwanza kwenda mikoa mbalimbali hapa nchini.
Kutokana na kazi yangu hivyo nilikuwa nasafiri mara kwa mara. Mwaka 2019 mdogo wangu wa kiume alihitimu kidato cha sita kisha nikaamua kumleta nyumbani ili aweze kusaidiana na mke wangu dukani.
Nilimtumia nauli ya kutoka kijijini kwetu hadi Mwanza kisha nikamtumia dereva wangu akampokea stand ya Nyegezi. Alifika salama nyumbani kwangu nikamuonesha chumba cha kulala.
Jinsi biashara ya nguo inavyoenda dukani.Walisaidiana na mke wangu pamoja na wafanyakazi wengine katika kufanya shughuli zao za kila siku.Kwa Upande wangu mimi nilikuwa siendi dukani mara kwa mara japo nikipata muda nilikuwa nawatembelea na kuona jinsi gani biashara inavyoenda.
Mwezi mmoja kupita tulifanya mahesabu ya mwezi nikaona kuwa biashara inakuwa kwa kasi kubwa sana kutokana na ushirikiano wa mke wangu na mdogo wangu, nikaamua kuongeza millioni 3 tena katika hiyo biashara hivyo wakaanza kuuza jumla na rejareja kwa wateja wao.
Kutokana na kupanda kwa biashara kila mwezi mdogo wangu Roja arikuwa anapata laki 3 kwa ajili ya matumizi yake binafsi.Nilifanya hivyo ili mdogo wangu asikose kitu chochote anachokihitaji pia kupitia nafasi hiyo aweze kuanzisha biashara yake mwenyewe muda ukifika kutokana na matokeo yake ya kidato cha sita hayakumpatia nafasi ya kujiunga na masomo ya elimu ya juu.
Mke wangu Juriana na mdogo wangu Roja waliweza kuwa karibu sana kutokana na kufanya biashara pamoja ila kwa upande wangu sikuweza jua kama kuna kitu kinaweza endelea kati yao zaidi ya biashara tu.
Mimi niliendelea na safari zangu za mara kwa mara kama kawaida yangu nikimuacha mke wangu na mdogo wangu wakiendelea na kazi zao.
Siku moja nilitoka safari kisha nikawapitia dukani na kuwasubiri wafungue muda ukiwadia ili turejee nyumbani wote. Muda ulitimia kisha wakafunga duka na tukarudi nyumbani.
Tulipofika nyumbani niliweza pumzika kidogo na mke wangu na badaye nikaenda chumbani kwa mdogo wangu Roja kwa ajili ya kumpatia nguo zangu aninyoshee ambazo nitavaa kesho yake asubuhi.
Baada ya kumkabidhi nguo zangu alitoa shuka la kutumia kwa ajiri ya kunyoosha nguo ndipo niliona chupi ya mke wangu kitandani kwake.
Nilipomuuliza chupi ya mke wangu inafanya nini kitandani kwake akasema hata yeye hajui nani kaileta kwenye chumba chake. Mimi nilichukua ile chupi hadi chumbani kwetu kisha nikafikiria tukimaliza kula nimuulize mke wangu.
Baada ya chakula tulianza mbadirishano wa mawazo na mke wangu ndipo nikamuonesha chupi yake na kumuuliza ilikuwa inafanya nini kwa chumba cha Roja.
Mke wangu alicheka kisha akaniambia kuwa mtoto wetu Rita ndo ana tabia ya kubeba nguo zake kutoka chumbani kwa sababu ameanza kutembea,hivyo kila anachokutana nacho anabeba tu. Sikuweza mkatalia mke wangu kutokana na maelekezo aliyonipatia ila moyo wangu ulibaki na wasiwasi na kujiuliza mbona mtoto wangu Rita hakubeba nguo nyingine zaidi ya chupi, kama amebeba chupi mbona hajaiweka sebuleni.
Kutokana na hayo maswali ilinibidi nianze kuwafuatilia mke wangu na mdogo wangu bila wao kujua. Ndipo siku moja nikamwambia mke wangu kuwa nasafiri kwenda Karagwe kwa ajili ya kununua maharagwe hivyo ntakaa kule siku saba, ila mimi sikuweza fika Karagwe bali nilibaki Mwanza ili nijue nikitoka kipi uwa kinaendelea nyumbani.
Baada ya siku tatu nilirudi nyumbani usiku bila wao kunitarajia kisha nikamuomba mdogo wangu Roja simu yake kisha nikaenda moja kwa moja kwa WhatsApp na kukutana na picha za uchi za mke wangu pamoja na messages walizokuwa wanatumiana, hapo ndo nilijua kuwa walikuwa wanashiriki tendo la ndoa kwa muda mrefu hata chupi kuwepo kwa chumba ya Roja siyo mtoto wangu Rita alichukua kule.
Je nifanye nini, nimfukuze mke wangu au nimfukuze mdogo wangu? Je nikimfukuza mdogo wangu nyumbani watanifikiliaje hali ya kuwa baba yetu alifariki na kuniomba niwalee wadogo zangu. Naomba ushauri wenu.
Kiwangadoctors wana dawa ya kurudisha mpenzi wako aliyekuacha,dawa ya Nguvu za kiume, dawa ya kusafirisha nyota yako,dawa ya mvuto wa biashara,dawa ya kupata kizazi,dawa ya mapenzi pamoja na dawa ya kushinda michezo ya batinasibu.
Wasiliana na kiwangadoctors kwa namba ya simu +254 769404965, barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. Pia unaweza tembelea website yao www.kiwangadoctors.com kupata taarifa zaidi na jinsi wanavyosaidia watu.
0 COMMENTS:
Post a Comment