August 5, 2021



NYOTA Mpya wa Simba, Yusuph Mhilu kwa msimu wa 2020/21 ndani ya Ligi Kuu Bara ametupia jumla ya mabao 9 kati ya 38 ambayo yalifungwa na timu hiyo.

Alikuwa ni namba moja kwa utupiaji na bao lake la kwanza alifunga mbele ya KMC, ilikuwa Uwanja wa Kaitaba zama za Mecky Maxime ambaye alichimbishwa mazima kazi ndani ya timu hiyo.

Kwa sasa Mhilu ni mali ya Simba ambapo alikuwa anatajwa pia kurejea kwenye timu yake ya zamani ya Yanga mambo yakawa tofauti baada ya mabosi wa Simba kumpa dili la miaka mitatu.

Unakuwa ni usajili wa pili kwa Simba msimu huu baada ya ule wa kwanza wa Peter Banda kutangazwa na sasa ni zamu Mhilu.

Nyota huyo ndani ya Kagera Sugar ameyeyusha jumla ya dakika 2,142 alizocheza kwenye Ligi Kuu msimu wa 2020/2021 kati ya mechi 34 ambazo timu hiyo ilicheza.

Kwenye msimamo timu ya Kagera Sugar ilimaliza ikiwa nafasi ya 12 na pointi zake 40 inanolewa na Kocha Mkuu Francis Baraza.

Anaungana na nahodha wake aliyekuwa naye kwenye timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, John Bocco mwenye mabao 16 akiwa ni mfungaji bora kwa msimu wa 2020/21.

5 COMMENTS:

  1. Kauze sura sio kucheza wazee wakuuwa vipaji

    ReplyDelete
  2. Moja ya vijana hazina kubwa kabisa ya soka nchini. Simba wamelamba Dume kweli kweli. Wanaosema Muhilu anakwenda kuua kipaji chake Simba ni wapumbavu.Simba ni mlima wa mafanikio kwa mpira wetu wa Tanzania kila mchezaji anatamani kufika pale. Mchezaji akifika pale akibweteka ataanguka kweli vibaya tu lakini akikaza basi kupaa angani ni Kama kunywa maji na hahihalisi anacheza nafasi gani mwenye kujitahidi kufanikiwa Mbawna Samara yupo wapi hivi sasa? Muhilu ni zao la Yanga akiwa kinda kabisa lakini wakamtelekeza leo kaenda Simba maneno ya chuki yamekuwa mengi, watanzania tuache roho mbaya tunatakiwa kuombeana mazuri.

    ReplyDelete
  3. Salamba, Miraji, Ndemla, Gadiel, Dida, nk

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona husemi boko,nyoni,mzamiru,shabalala,manula,kapombe,mkude,kenedy,acha kukariri brother,hatuko shule za kata hapa.mane iz beta zan edukesheni

      Delete
  4. Kila mchezaji anatamani kucheza Simba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic