KLABU ya Simba imemtambulisha nyota mpya mwingine mzawaeo Agosti 18 kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo kwa msimu wa 2020/21.
Ni Jimmyson Steven Mwanuke mwenye umri wa miaka 18 ambaye alikuwa anakipiga ndani ya Gwambina FC.
Anauhakika wa kushiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao kwa kuwa timu ya Gwambina FC ya Mwanza itashiriki Ligi Daraja la Kwanza baada ya kushuka msimu uliopita.
Ilimaliza ikiwa nafasi ya 16 ilikusanya pointi 35 baada ya kucheza jumla ya mechi 34 anakuwa mali ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes na ilitwaa taji la Ligi Kuu Bara baada ya kufikisha pointi 83.
Dili la Steven ambaye ni winga inaelezwa kuwa ni miaka mitatu na atakuwa hapo mpaka msimu wa 2024.
Huyu ni nyota wa nane kutambulishwa Simba anaungana na Henock Baka, Peter Banda, Duncan Nyoni, Pape Ousmane, Yusuph Mhilu,Israel Patrick na Abdulsamad Kassim.
Huo sasa usajili mpya sio kuziba mapengo tunaanza wote kuijenga timu
ReplyDeleteMoja ya sajili inayovutia ya simba zaidi ni hii ya huyu Dogo kwani sio mazoea kwa klabu zetu hizi kujipa kazi ya kuibua na kulea vipaji ila kwa Sasa Simba inaonekana imedhamiria business zaidi.Asanteni Sana wekundu wa msimbazi ila Dogo aendelezwe ipasavyo anauwezo wakuja kufanya maajabu licha umri Wake kuwa Mdogo, Samata alifanya hivyo ndani ya Simba.
ReplyDeleteWacha utopolo wakereke na usajili wa simba walidhani Simba itabweteka.Utopolo walifanya usajili wao kwa kukiangalia kikosi like cha Simba ongezea bila ya Chama bila Miqisone. Lakini Mara pa😀
ReplyDeleteSimba anafanya usajili kamili. Utopolo lazima wapaniki wasonye msonyo wa shetani si walaumu☹️
Kwel we shabik anus zaid tanzania iv mchezaj kasajiliwa cmba kwn mpak uitaje yanga au?
DeleteMpaka uitaje yanga?muda tuu utaongea
DeleteKumbe yanga imetajwa hapo? Hahahaaa, mi sijaona
DeleteMika bwan
ReplyDeleteVinawashwa Ni Kama Wanawake bila Vikao vyao lazima wataje Wanaume.
ReplyDelete