August 30, 2021

MZEE Sunday Mnara, baba mzazi wa Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara ambaye ni ingizo jipya kutoka Simba, amesema kuwa kufungwa kwenye mchezo wa majaribio ni jambo la kawaida kwa kuwa jana kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Zanaco.

 Amesema kuwa ukweli ni kwamba uongozi wa Yanga unatakiwa kukaa na benchi la ufundi ili kuweza kuongea naye ili waweze kushinda kwa kuwa hawakustahili kushindwa.

 

7 COMMENTS:

  1. Naamini khaji kwenda Yanga ndio mahala pake na wanayanga wampokee atulie nyumbani.kuhusu kuonewa khaji ni vitu vya kufikirisha Sana.
    Nnavyoamini mimi, hizi timu licha ya utani wa jadi kuna miiko na mipaka wahudumu wa hizi club hutakiwi hata kuikarabia kuivuka. Mzee Manara mwenyewe anajua. Huwezi kuwa mtu wa kaliba ya uongozi wa hizi timu halafu uwe na vikao vyako binafsi na viongozi wa upande wa pili hasa wakati ambao timu hizi mbili zinapoelekea kwenye mechi baina yao. Yawezekana viongozi wa Yanga walikuwa wakicheza mind game zidi ya Simba kwa kupitia Manara au walikuwa na mambo yao mengine na Manara ila ninavyofahamu mimi kiongozi wa Yanga anatakiwa Yanga kweli kweli na kiongozi simba anatakiwa kuwa kiongozi wa Simba kweli kweli bila kupepesa macho ndio utamaduni wetu na sio rahisi kukiondoa hicho kitu mara Moja.
    Kuhusu madai ya kuonewa Manara ndani ya Simba sidhani kama ni busara kutoa shutuma hizo kwenye mitandao ni jambo la busara. Nchi yetu ni nchi inayofuata utawala wa Sheria na taratibu za kazi.Kuna taasisi maalum za kisheria na za kiserikali kwa mfanya kazi au mtumishi aliekuwa hakutendewa haki na mwajiri wake kwenda kuwasilisha malalamiko yake na huo ndio utaratibu karibu Duniani kite kuliko kujikita katika kuchafua kwenye mitandao ya kijamii na khaji Manara sio Malaika kuwa yeye huwa anafanya mazuri tu hana mabaya ni Kwakuwa tu uongozi wa Simba umeamua kuwa weledi kwa kutolipiza kisasi kwenye majibizano kwenye mitandao.

    ReplyDelete
  2. Simba hawawezi kujibizana naye kwani atatoa siri kubwa zaidi (ambazo ana ushaidi) ndio maana wameku wa wapole.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sio simba hawawezi kujibizana nae bali simba wameamua kuwa busys na timu yao zaidi. Ukijibizana na muendawazimu utakuwa huna na tofauti na yeye.Khaji na hasira zake zile kama angekuwa na siri asingesubiri jua lichwe kabla kuzimwaga ziwe za kweli ziwe za kutunga.

      Delete
  3. Kujibizana na kuumbuwana hakuleti kheri isipukuwa mikosi na maafa. kwasababu maumivu yatokanayo na ulimi yanaumiza kuliko majaraha ya upanga na neno jema linamtowa nyoka pangoni

    ReplyDelete
  4. Ninawaomba Wana Simba kuendelea na ile siyasa ya kutojibizana ambayo ni siasa ya uungwana na ushindi tunaoutaka sio wa nani hodari wa kusema lakini ni ule wa kuendelea na makombe

    ReplyDelete
  5. Haji amezoea tabia za kike za kusutana na kuchambana.Nani ana muda wa kubishana na mpiga debe kama alivyowahi kusema Nugaz.Anatembelea brand za timu hizi mbili.Aujaze uwanja kwenye mechi ya Azam waajiri wake pia na Biashara ndio wstu wazungumzie kipaji.

    ReplyDelete
  6. Naunga mkono hoja.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic