August 30, 2021

 


LIVERPOOL kwa sasa ni timu pekee ndani ya Ligi Kuu England ambayo inapewa  nafasi ya kuipata saini ya mshambuliaji wa Tottenham na nahodha wa timu ya taifa ya England, Harry Kane ambaye awali alikuwa anatajwa kuibukia ndani ya Manchester City ila dili likabuma.

Kwa mujibu wa kocha wa zamani wa Tottenham, Tim Sherwood amebainisha kwamba licha ya City kushindwa kuipata saini ya Kane ambaye aliweka wazi kwamba anahitaji kubaki ndani ya timu hiyo ni Liverpool pekee ambayo inaweza kupata saini ya mshambuliaji huyo.


Liverpool wanapewa nafasi ya kuipata saini ya nyota huyo kwa kuwa Kocha Mkuu, Jurgen Klopp anataka kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji kwa kuwa ana hasira na mafanikioyaliyotokana na kuboronga kwake msimu uliopita kwenye ligi.



1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic