August 2, 2021

JANA Yanga ilicheza mchezo wa ufunguzi na Big Bullets ambapo ulikuwa ni wa Kombe la Kagame, mashabiki wameweka wazi kwamba Yanga ni timu kubwa na malengo ni kushiriki kwenye kila mashindano na kushinda.

 Kuhusu kiwango cha jana baada ya ubao kusoma 1-1 bado wameweka wazi hakijawa bora huku wakiweka wazi kwamba mechi zijazo watafanya vizuri. Kuhusu watani zao wa jadi Simba wameeleza kuwa wamewazidi kwenye kila kitu.

 

6 COMMENTS:

  1. Huyu ni mwehi wala hajui mpira. Unadharau super cup ya caf unasema hili bonanza la cecafa ndio bora? Kichekesho. Simba iko namba 12 africa yanga hata top 100 haimo. Sasa unaidharau vipi. Tunachoshana tuu. Timu inalimwa yellow zaidi ya 10 na red juu huoni kuwa ni magumashi na vurugu tuu hakuna ufundi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Timu serious ya levo ya klabu bingwa haifanyi utani kunako usajili. Wanachokifanya Yanga na majaribio yao wachezaji wanaotaka kuwasajili ni ujinga na timu jinga itafeli tu. Angalia Azam wamesajili wachezaji kamili waliowanyia skauti tayri na wanachokifanya hivi sasa Kama wapo kwenye precamp.
      Simba wapo kimya ila Simba wapo kamili gado sio mbaya Kama wataongeza beki mwengine jiwe wa Kati kuimarisha backline yao kimataifa. Yanga kelele za hovyo ndio zao mwisho wa siku wanakuja kufurahia kutoa sare na Simba.

      Delete
  2. Msimu ndo kwanza unakaribia kuanza, haya mnayoyasikia sio mageni kila msimu ndo hivi hivi utasikia timu itaimarika na raundi ya kwanza ikifika katikati utasiki sasa ndo tunaanza ligi halafu eti mtu huyo na anataka ubingwa wakati mwenzake kuanzia mwanzo anafanya vizur.... Mpira wa mdomoni ifike wakati muachane nao la sivyo mtasubiri sana

    ReplyDelete
  3. Nilisha sema wakienda kimataifa na timu lao la kucheza judo watakula nyingi tu kule hakuna marefa wenye unazi

    ReplyDelete
  4. Bullets zimemrusha akili huyo na wamekuwa wakiweseka ovyo

    ReplyDelete
  5. Kwani Yanga wageni Kimataifa,na je hiyo michuano ya CECAFA siyo ya Kimataifa?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic