August 22, 2021

 


TAARIFA kutoka nchini Morocco zinasema kuwa upo uwezekano mkubwa wa klabu ya Yanga kucheza mchezo wa kirafiki na klabu ya Raja Casablanca, wakiwa huko nchini Morocco mara baada ya klabu hiyo kupokea maombi kutoka kwa timu mbili za nchini humo kuhitaji kucheza na Yanga.

Yanga kwa sasa ipo nchini humo ambapo watakaa kwa siku 10 kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao kisha kurejea nchini, tayari kwa ajili ya siku ya kilele cha wiki ya mwananchi ambayo inatarajiwa kufanyika Agosti 29.

Chanzo chetu cha ndani kutoka Yanga kimetuambia kuwa klabu ya Raja Casablanca kutoka Morocco, ni moja kati ya timu ambazo zimepeleka maombi kwa ajili ya kukipiga na Yanga ikiwa ni maandalizi kwao kwa msimu ujao.

“Klabu ya Raja Casablanca tayari wameomba mchezo wa kirafiki na Yanga kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao hivyo inawezekana mchezo huo ukafanyika au usifanyike kutokana na maamuzi ya benchi la ufundi kama litahitaji mechi hiyo ifanyike,” kimesema chanzo hiko.

Alipotafutwa Injinia Hersi Said ambaye alikuwa ni mwenyekiti msadizi wa kamati ya usajili ya Yanga amesema: “Ni kweli kuna maombi ya timu mbili kutoka Morocco ambazo zimewasilisha tayari maombi ya kucheza na sisi, lakini hilo tumelipeleka kwa benchi la ufundi kama watakubali basi mechi inaweza ikawepo.”

 

 

19 COMMENTS:

  1. Acheni kucheza msije mkatia aibu bure

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nyie si mlikibizwa vipindi vyote viwili mkatoa draw Kwa goli la kuotea. Kocha akabakia kusema 'but, but' hehehe

      Delete
  2. Kabisa Yanga wakikubali tu wamekwisha wiki ya wananchi itageuka kuwa wiki ya majonzi

    ReplyDelete
  3. Kwa hivyo Yanga wamekaa mkao wa tonge wakisubiri sapraiz ya kumtambulisha Manara ndani ya Yanga kwenye siku ya wananchi? Naona Yanga ikienda kupasuka kwenye hili la Manara.Baada ya kuondoka Manara ndani ya Simba kumekuwa pahala pa amani Sana.Na sasa imekuwa dhahiri Sana kuwa Manara alikuwa akiwahujumu Simba kwenye mechi na Yanga.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaani Mikia Fc bhana, habari inahusu Mechi ya Yanga na Raja Cassablanca, sasa wapi na wapi comments zinazomhusu Haji Manara? Achei mchecheto

      Delete
    2. Fumbua macho uone, leo Manara ndio wakuihujumu Simba? Kweli mikia fc ni akili ndogo inayoburutwa na familia ya mudi. Acheni unafiki, subirini ukweli ujidhihirishe

      Delete
    3. Mtajua anayewakera ni Manara au mudi, acheni kumtukuza mudi mkawadharau wazalendo kwa sababu ya umaskini wenu. Ukweli mnaujua kuwa anayewadhamini anawahadaa ila mnaogopa kuisema kwa sababu atawaacha

      Delete
  4. Manara alikuwa msaliti mkubwa kwenye mechi na Utopolo. Na angekuwepo tungefungwa.

    ReplyDelete
  5. Najua Utopolo wataogopa kucheza na casablanca

    ReplyDelete
  6. Ni ukweli tumekuwa tukimtumia Manara kuihujumu simba kwa muda mrefu sana. Lakini huyu bi dada tumebaini ni kachero. Hata hivyo wanayanga msiwe na waswas tutaweka mtu mwengine ndani ya simba hivi karbuni.

    ReplyDelete
  7. Ndio mna tamaa ta kupata nini. Mlikuwa na watu kana mnavojidai lakini nini mlichokipata isipokuwa kukosa kila kitu hata Morrison mnaemngojea inaonesha mmeshatiwa kapuni

    ReplyDelete
  8. Hakuna mwingine zaidi ya MO, timu imekaa vizuri kushiriki kwa kuonesha ushindani mashindano ya afrika mpaka utopolo mkaenda kwa nafasi ya viti maalumu klabu bingwa afrika, hersi said mlimbeba kwenye machela, hiyo hali c alishawaona nyie misukule

    ReplyDelete
  9. Fanyeni utopolo c kuchezesha viuno kambini tu

    ReplyDelete
  10. Mikia Mikia hivi mna nn lakini yn Leo hii manara kawa msaliti aiseeh kweli walimwengu hawana maana

    ReplyDelete
  11. Breaking: Yanga wameamuwa kurudi kwa makundi kuanza leo ikionesha ile mechi ya kujipima ikiota mbawa na visababu visivoingia akilini mojawapo Morocco joto kali sana, jee joto hilo ni kwao tu na wala si kwa Simba ambao wameamuwa kurefusha kuepo huko ili ipate mechi zaidi za kujipima.

    ReplyDelete
  12. Yanga mnakurupukaga sana ila ngoja tusubiri muda,kwa takribani misimu mitatu mfululizo yanga imekua ikikurupuka sana kwenye suala la usajili yani inapuyanga kama vile haina macho.hatuisemei mabaya ila tumeona athari kubwa mbaya waliopata yanga,wengi watalinganisha simba na yanga bila kuangalia mafanikio ya simba,tunaomba unapotoa coment plz linganisha na mafanikio ambayo simba wamepata,ni mtazamo tu ila ukweli ndio huo yanga imekua ya ajabu sana,watu wanakuja nakuondoka kama stendi ya daladala.kueni makini jamani.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic