August 22, 2021

KAIMU Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ezekiel Kamwaga ameweka wazi kuwa ataondoka katika nafasi hiyo mara tu baada ya muda aliopewa wa miezi miwili kukaimu kukamilikia.

Julai 28, mwaka huu Bodi ya Wakurugenzi ya Simba ilimtangaza rasmi Ezekiel Kamwaga kushika nyadhifa ya Kaimu wa Idara ya habari na mawasiliano wa klabu hiyo, kuifuatia kuondoka kwa aliyekuwa Msemaji wa Simba, Haji Manara.

Akizungumzia majukumu yake ndani ya Simba, Kamwaga amesema: “Watu wengi wanauliza kwanini nimekaimu nafasi hii kwa miezi miwili pekee, licha ya kwamba nina uzoefu wa kutosha wa kusalia kwa muda mrefu zaidi, na labda ikiwa nitaendelea na majukumu haya baada ya muda niliopewa kukamilika.

“Lakini ningependa kuweka wazi makubaliano yangu na Uongozi wa juu wa Simba ni kushikilia nafasi hii kwa miezi miwili, na siwezi kuongeza hata siku moja mara baada ya muda huo kukamilika.

“Hii ni kwa sababu nina majukumu yangu binafsi ambayo natakiwa kuyafanya nje ya Tanzania, lakini kabla ya kuondoka ni lazima nihakikishe nimekamilisha kazi ya kufanikisha mchakato wa kumtafuta msemaji mpya.”

 

 

3 COMMENTS:

  1. Mikia Kwa midomo, too much!

    ReplyDelete
  2. Mbona kichwa cha habari hakiendani hata na ulichoandika kwenye habari? Au ndyo kuwatafuta wateja. Mimi habari zako sijawahi kuzielewa hata siku moja. Pumba tu kila siku.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwan umelazishwa kufutilia habari zake

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic