TAARIFA kutoka nchini Morocco zinasema kuwa upo uwezekano mkubwa wa klabu ya Yanga kucheza mchezo wa kirafiki na klabu ya Raja Casablanca, wakiwa huko nchini Morocco mara baada ya klabu hiyo kupokea maombi kutoka kwa timu mbili za nchini humo kuhitaji kucheza na Yanga.
Yanga kwa sasa ipo nchini humo
ambapo watakaa kwa siku 10 kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao kisha kurejea
nchini, tayari kwa ajili ya siku ya kilele cha wiki ya mwananchi ambayo
inatarajiwa kufanyika Agosti 29.
Chanzo chetu cha ndani kutoka Yanga
kimetuambia kuwa klabu ya Raja Casablanca kutoka Morocco, ni
moja kati ya timu ambazo zimepeleka maombi kwa ajili ya kukipiga na Yanga ikiwa
ni maandalizi kwao kwa msimu ujao.
“Klabu ya Raja Casablanca tayari wameomba
mchezo wa kirafiki na Yanga kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao hivyo
inawezekana mchezo huo ukafanyika au usifanyike kutokana na maamuzi ya benchi
la ufundi kama litahitaji mechi hiyo ifanyike,” kimesema chanzo hiko.
Alipotafutwa Injinia Hersi Said
ambaye alikuwa ni mwenyekiti msadizi wa kamati ya usajili ya Yanga amesema: “Ni kweli kuna maombi ya timu mbili kutoka Morocco ambazo zimewasilisha tayari
maombi ya kucheza na sisi, lakini hilo tumelipeleka kwa benchi la ufundi kama
watakubali basi mechi inaweza ikawepo.”







Acheni kucheza msije mkatia aibu bure
ReplyDeleteNyie si mlikibizwa vipindi vyote viwili mkatoa draw Kwa goli la kuotea. Kocha akabakia kusema 'but, but' hehehe
DeleteKabisa Yanga wakikubali tu wamekwisha wiki ya wananchi itageuka kuwa wiki ya majonzi
ReplyDeleteKwa hivyo Yanga wamekaa mkao wa tonge wakisubiri sapraiz ya kumtambulisha Manara ndani ya Yanga kwenye siku ya wananchi? Naona Yanga ikienda kupasuka kwenye hili la Manara.Baada ya kuondoka Manara ndani ya Simba kumekuwa pahala pa amani Sana.Na sasa imekuwa dhahiri Sana kuwa Manara alikuwa akiwahujumu Simba kwenye mechi na Yanga.
ReplyDeleteYaani Mikia Fc bhana, habari inahusu Mechi ya Yanga na Raja Cassablanca, sasa wapi na wapi comments zinazomhusu Haji Manara? Achei mchecheto
DeleteFumbua macho uone, leo Manara ndio wakuihujumu Simba? Kweli mikia fc ni akili ndogo inayoburutwa na familia ya mudi. Acheni unafiki, subirini ukweli ujidhihirishe
DeleteMtajua anayewakera ni Manara au mudi, acheni kumtukuza mudi mkawadharau wazalendo kwa sababu ya umaskini wenu. Ukweli mnaujua kuwa anayewadhamini anawahadaa ila mnaogopa kuisema kwa sababu atawaacha
DeleteManara alikuwa msaliti mkubwa kwenye mechi na Utopolo. Na angekuwepo tungefungwa.
ReplyDeleteNajua Utopolo wataogopa kucheza na casablanca
ReplyDeleteNi ukweli tumekuwa tukimtumia Manara kuihujumu simba kwa muda mrefu sana. Lakini huyu bi dada tumebaini ni kachero. Hata hivyo wanayanga msiwe na waswas tutaweka mtu mwengine ndani ya simba hivi karbuni.
ReplyDeleteNdio mna tamaa ta kupata nini. Mlikuwa na watu kana mnavojidai lakini nini mlichokipata isipokuwa kukosa kila kitu hata Morrison mnaemngojea inaonesha mmeshatiwa kapuni
ReplyDeleteHakuna mwingine zaidi ya MO, timu imekaa vizuri kushiriki kwa kuonesha ushindani mashindano ya afrika mpaka utopolo mkaenda kwa nafasi ya viti maalumu klabu bingwa afrika, hersi said mlimbeba kwenye machela, hiyo hali c alishawaona nyie misukule
ReplyDeleteDezo dezo fc wazee wa utopolo
ReplyDeleteFanyeni utopolo c kuchezesha viuno kambini tu
ReplyDeleteMikia Mikia hivi mna nn lakini yn Leo hii manara kawa msaliti aiseeh kweli walimwengu hawana maana
ReplyDeleteBreaking: Yanga wameamuwa kurudi kwa makundi kuanza leo ikionesha ile mechi ya kujipima ikiota mbawa na visababu visivoingia akilini mojawapo Morocco joto kali sana, jee joto hilo ni kwao tu na wala si kwa Simba ambao wameamuwa kurefusha kuepo huko ili ipate mechi zaidi za kujipima.
ReplyDeleteUto kwao pemba
ReplyDeleteYanga mnakurupukaga sana ila ngoja tusubiri muda,kwa takribani misimu mitatu mfululizo yanga imekua ikikurupuka sana kwenye suala la usajili yani inapuyanga kama vile haina macho.hatuisemei mabaya ila tumeona athari kubwa mbaya waliopata yanga,wengi watalinganisha simba na yanga bila kuangalia mafanikio ya simba,tunaomba unapotoa coment plz linganisha na mafanikio ambayo simba wamepata,ni mtazamo tu ila ukweli ndio huo yanga imekua ya ajabu sana,watu wanakuja nakuondoka kama stendi ya daladala.kueni makini jamani.
ReplyDeleteUNARUHUSU POVU?
ReplyDelete