UONGOZI wa Yanga umeeleza kuwa sababu kubwa ya kuachana na nyota zao wawili ambao ni makipa ni kufuata ripoti ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.
Ni Metacha Mnata na Faroukh Shikalo ambao wote kandarasi zao zilikuwa zimemeguka na Nabi hakuwa tayari kuona wakiongezewa mkataba.
Kwa mujibu wa Haji Mfikirwa, Kaimu Katibu wa Yanga amesema kuwa ilikuwa ni mapendekezo ya kocha kuachana na wachezaji hao wote wawili.
"Tunafanya kazi kwa kuzingatia ripoti ya mwalimu hivyo ni yeye ambaye alipendekeza tufanye hivyo na hakuna namna nyingine.
"Mnata yeye amepewa barua leo ya kuwa mchezaji huru hivyo tunamtakia kila la kheri pamoja na Shikalo," amesema.








Binafsi nimesikitishwa kwa kuachwa kwa Faroukh Shikalo lakini si kwa yule muuza duka
ReplyDeleteNa usajili wa Ajibu nao ni ushauri wa kocha Nasridine? Kamuona wapi akicheza? Acheni kuwazuga watu. Kwa Metacha mmepoteza bonge moja la Goal keeper. Timu Kama biashara wanapaswa kumdaka Metacha juujuu. Pia Metacha Hana Cha kupoteza wanaomsimia wajaribu kumtafutia timu nje japo madaraja ya chini kwenye nchi zilizo songa mbele kimpira hata hapa Africa.
ReplyDeleteKamuona kwenye video
DeleteWameshindwa kuambakisha shikalo kwani watakua na ma golikipa wawili wa kigeni. Kwa Metacha yeye ni sawasawa kuachwa, hilo lilikua ni duka la Simba.
ReplyDeleteAchana na mawazo finyu, Simba ndo walikuwa wanamtumia bila kumlipa?
DeleteKama Haji Manara
DeleteMjiandae kusajili kipa mwingine dirisha dogo la sivyo mtajuta
ReplyDeleteSwala la usajili kinawahusu Yanga, wengine fanyeni yenu
ReplyDeleteHata huyo Kocha Nabi achunguzwe
ReplyDeleteAma huyo Faruku anatia huruma. Juu ya kiwango kikubwa alichokionesha na mapenzi yake makubwa kwa yanga na kuwa ni yeye ndie aliefsnikisha usajili wa huyo Khalid wa Uganda na kuonesha chuki zake kwa Simba, lakini yote hayo hayakumsaidia kitu, kangolewa kama jino bovu bila ya kupigwa shindano
ReplyDeleteSafi sana kuacha na dukanla rejareja aka Mechata Mnata, sasa waliokuwa wanamnunua wamsajili na ndio itakuwa funzo kwa vijana wengine. SHIKALO aliomba mwenyewe kuondoka ila pia kwa muda ameshindwa kuwa mwepesi hasa akichunguliwa any way will miss you Shikalo umefanya mazuri Yanga.
ReplyDeleteHata huyo mpya ni duka la Simba Kama unabisha subiri septemba 25
ReplyDeletekwani mukoko atapewa kadi nyekundu tena?
DeleteAkicheza judo baada ya kuzidiwa soka anapewa haki yake
Delete