September 10, 2021


 KLABU ya Arsenal imeweka rekodi mbovu kwa mechi za mwanzo ndani ya Ligi Kuu England kwa kushindwa kukusanya pointi hata moja pamoja na bao ndani ya uwanja.


Ikiwa imecheza jumla ya mechi tatu za Ligi Kuu England haijafunga bao hata moja rekodi inayowapasua kichwa washambuliaji wake pia hata benchi la ufundi.

Timu hiyo pendwa Ulaya imefungwa mabao 9 ambayo ni mengi na mchezo wao dhidi ya Manchester City uliochezwa Agosti 28 walikubali ubao wa Uwanja wa Etihad kusoma Manchester City 5-0 Arsenal.

Pia katika mchezo huo uliwafanya Arsenal waweze kushuhudia kadi moja nyekundu iliyoonyeshwa kwa Granit Xhaka ilikuwa dk ya 35.

Rekodi nyingine mbovu ambayo ilikusanywa na Arsenal ni ile ya kupiga shuti moja na halikuweza kulenga lango huku wapinzani wao Manchester City wakipiga mashuti 25 na mashuti 10 yalilenga lango.

Ni rekodi mbovu ya Kocha Mkuu Mikel Arteta kwa kuwa amekuwa na ukuta nyanya safu ya ushambuliaji inayoongozwa na nahodha Pierre Aubameyang ikiwa ni butu kinomanoma ndani ya uwanja msimu huu.

Kwa sasa ni Westham United na Manchester City zinaongoza kwa kufunga mabao mengi ambayo ni 10 kwa kila timu zote zimecheza mechi tatutatu.

Timu tatu zikiongozwa na Arsenal hazina pointi kibindoni nyingine ni Wolves na Norwich City zimefungwa mechi zote tatu jambo linalowafanya wawe katika mtihani wa kujiondoa kwenye hatari ya kuwachimbisha makocha wao.

Kwenye tatu mbovu ni Norwich City iliyo nafasi ya 19 imefunga bao moja huku Arteta akiwa katika wakati mgumu na anatajwa kuwa miongoni mwa makocha ambao watachimbishwa mapema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic