September 18, 2021

 


AZAM FC leo imeibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Horseed FC ya Somalia katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Ni bao la Isamil Kader alipachika bao pekee la ushindi dakika ya 38 kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Horseed FC ya Somalia.

Mchezo wa leo kipindi cha kwanza Azam FC waliweza kupata ushindi huo na kipindi cha pili ngoma ilikuwa nzito kwa timu zote kuweza kupata bao.

Azam FC inasonga hatua inayofuata na itakutana na Pyramids FC katika mchezo wao ujao huku wapinzani wao Horseed FC wakigungashiwa virago.

Ushindi wa jumla ni Horseed FC 1-4 Azam FC. Vivier Bahati Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa wanahitaji kufanya vizuri hatua inayofuata.

2 COMMENTS:

  1. Hapo kwa Pyramids FC wakaze la cvo hawatafikia record ya namungo hadi kwenye makundi

    ReplyDelete
  2. uwekezaji wa pyramid hata tykiunganisha timu tatu zetu za juu hatuwapati, sasa msitegemee kuwashinda kirahisi hao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic