September 10, 2021

 


KIUNGO wa kimataifa wa Kenya na klabu ya Azam, Kenneth Muguna tayari ameripoti kwenye kambi ya Azam, kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya klabu ya Horseed kutokea nchini Somalia.

Muguna ni miongoni mwa nyota wa Azam ambao walikosekana kwenye maandalizi ya mwisho ya Azam katika kambi yao ya wiki moja na nusu iliyokuwa nchini Zambia kwa ajili ya maandalizi ya kabla ya msimu ‘Preseason’, kutokana majukumu ya timu ya Taifa ya Kenya iliyokuwa na kibarua cha kucheza michezo ya kusaka tiketi ya kushiriki kombe la Dunia nchini Qatar mwakani.

Katika michuano hiyo ya kombe la Shirikisho Afrika azam inatarajia kucheza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya awali dhidi ya Horseed ya Somalia Septemba 11, mwaka huu katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam kabla ya kurudiana nao septemba 18, kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kutokana na sababu za kiusalama nchini Somalia.

Akizungumza kumhusu kiungo huyo, Mkuu wa Kitengo cha habari na mawasiliano wa Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ amesema: “Kikosi chetu kinaendelea vizuri na maandalizi ya mwisho kuelekea mechi ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Horseed ya Somalia, utakaochezwa siku ya Jumamosi.

“Tayari wachezaji wote ambao walikuwa wakikosekana kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo majukumu ya timu za Taifa wameripoti kambini kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.

“Hii inakuwa ni faida kubwa kwa kocha mkuu George Lwandamina kutokana na kupata nafasi ya kufanya mazoezi na kikosi chote kwa mara ya kwanza.”

 

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic