September 13, 2021


 MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Cristiano Ronaldo baada ya kucheza mchezo wake wa kwanza akiwa na uzi wa Manchester United alimliza mama yake baada ya kufunga mabao mawili.


Ronaldo alirejea Uwanja wa Old Trafford akitokea Juventus ikiwa ni baada ya miaka 12 kuyeyuka tangu aliposepa ndani ya timu hiyo ambayo kwa sasa inanolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer.

Mchezo wake wa kwanza Septemba 11 ilikuwa ni wa Ligi Kuu England na alitupia mabao mawili wakati timu yake ikishinda mabao 4-1 dhidi ya Newcastle United na mabao yale mengine yalifungwa na Jesse Lingard na Bruno Fernandes kwa upande wa Manchester United.


Baada ya kutupia mabao hayo mawili mamayake aitwaye Dolores Aveiro mwenye miaka 66 alishindwa kujiuzia baada ya kushangilia huku akitoa machozi ndani ya Uwanja wa Old Trafford.Inaelezwa kuwa Ronaldo alikuwa hafahamu kuwa mama yake atakuwa hapo kwa sababu alishakatazwa kutazama mechi wakati mwanaye akiwa anacheza.

 Kazi nyingine kwa Manchester United ni kesho Septemba 14 katika mchezo wa UEFA Champions itakuwa ni dhidi ya Young Boys.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic