September 8, 2021


 UNAWEZA kusema Yanga chini ya Kocha Mkuu, Nassredine Nabi, taratibu inaanza kunoga kutokana na timu hiyo kupata muunganiko mzuri hasa kwenye safu ya ushambuliaji ambayo inaongozwa na Heritier Makambo na Fiston Mayele.


Timu hiyo inayojiandaa na msimu wa 2021/22, 
tayari imecheza michezo minne ya kirafiki mpaka sasa ambapo imeshinda mitatu dhidi ya DTB (3-1), Friends Rangers (3-1) na Pan African (1-0), huku ikipoteza mmoja wa kimataifa dhidi ya Zanaco kwa kufungwa mabao 1-2.

 

Kwenye michezo hiyo minne, Yanga wameonesha muunganiko mzuri kwa wachezaji ambao utawasaidia kwenye michuano mbalimbali wakianza na Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali dhidi ya Rivers United ya Nigeria utakaochezwa wikiendi hii.


Msimu uliopita, Yanga ilionekana kuwa na shida 
kwenye safu ya ushambuliaji ambapo kwa sasa dawa inaonekana kupatikana kwani safu hiyo kwenye mechi nne ilizochezwa, imefunga mabao matatu.Mayele amefunga mabao mawili kwenye michezo dhidi ya Friends Rangers na Pan Africanhuku Makambo akifunga bao moja dhidi ya Zanaco.

 

Safu ya ushambuliaji ya Yanga inazidi kunoga kama ambavyo Kocha Nabi amekuwa akipambana iwe na makali ambapo hadi sasa inadhihirisha kwamba, siku akianzishwa mmoja, mwingine akiingia kutokea benchi ataendeleza makali yaleyale.

 

Lakini kama wakianzishwa wote, basi siku hiyo kutakuwa na balaa kubwa na mabeki wa timu pinzani watapata tabu sana wamzuie nane.

 

Yanga kwa sasa inacheza michezo ya kirafiki kwa ajili ya kujiimarisha zaidi katika kujiandaa na msimu ujao.Hivi karibuni, Nabi alinukuliwa akisema: “Kwa sasa natafuta muunganiko wa timu yangu kuanzia kwenye eneo la ulinzi, kiungo na ushambuliaji.

 

“Ukiangalia timu ina wachezaji wengi wapya ambao wanahitaji kuzoeana, hivyo kwa muda huu tunapaswa kuutumia vizuri ingawa naona vijana wameanza kuimarika.” Kuelekea mchezo wa Jumapili dhidi ya Rivers, Makambo amesema:

 

“Mashabiki mje kwa wingi siku ya Jumapili, tuje kuwajaza kwa pamoja, mkumbuke nyinyi ni wachezaji wa 12 uwanjani.”

5 COMMENTS:

  1. Tujaze uwanja ili mpate pesa mpira hamna pale msitufanye wajinga

    ReplyDelete
  2. Mjaze wewe na Nani kama Mpira hamna Kaa Nyumbani unawashwa na Nini?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kawatafutie ITC kwanza uongo tu. wewe unawashwa na ukweli

      Delete
  3. ITC Manake nini? kwani unadhani Ni Chakula?

    ReplyDelete
  4. Tunasubir ushindi tu hatutakianeno tunawamini wachezaji.waliopo ila ishu ya wachezaji waliozuiwa kucheza ikoje hadi SAS mayele nimuhimu.sana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic