September 14, 2021

 


JAVIER Tebas, Rais wa La Liga ameweka wazi kuwa kusepa kwa nyota wao wa zamani Lionel Messi katika ligi hiyo ni maumivu makubwa lakini ilikuwa haiwezi kuepukika kwa kuwa hata Barcelona wenyewe walikataa mbinu waliyopewa ili abaki.


Messi alishindwa kusaini dili jipya ndani ya timu yake ya Barcelona huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni sheria za La Liga katika matumizi ya mkwanja.


Licha ya nyota huyo kuwa tayari kupunguza mshahara wake kwa asilimia 50 mambo yalikuwa magumu kwake na amesepa kwa sasa yupo zake ndani ya kikosi cha PSG.


Tebas amesema kuwa waliwapa chaguo Barcelona ambalo lingewafanya abaki kwao ila walikataa mwisho wa siku ameacha maumivu katika La Liga.

"Kama wangekubali, Messi alikuwa na uwezo wa kubaki kuwa Barcelona wala asingeondoka,".

2 COMMENTS:

  1. Licha ya Messi kuondoka Ronald koeman ndio tatizo linalo tukumba wana Barcelona kocha hawezi kuifundisha timu kubwa kama hiyo huku hana hata kombe la mbuzi

    ReplyDelete
  2. Tumebaki nahumia sisi washabikiwa wa Barcelona ila kwa Sasa tumeamia PSG Kwa Sasa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic