September 10, 2021


KUPITIA teknolojia hakuna tena ambacho 
unaweza kukifanya siri zaidi ya kuyafanya mambo yaende kwa njia sahihi.

Teknolojia inakua na kuimarika kwa haraka sana hadi kufikia kutulazimisha kuongeza umakini kwa asilimia 100 kwa kila tunalolifanya leo.

Hali ilivyo ni hivi; kuna uhusiano mkubwa sana kati ya kile unachokisema leo na utakachokizungumza kesho. Vinaweza kuwa na muunganiko mkubwa na wa karibu sana na hii yote ni kuhusiana na suala la teknolojia.

Kasi ya ukuaji wa teknolojia umeifanya dunia kuwa kijiji, acha tu katika mawasiliano ya kawaida lakini imehamia hadi katika mawasiliano ya mazungumzo kwa kuwa si suala la upigaji simu pekee, badala yake unaweza kuwasiliana na mtu mwingine kupitia Whatsapp na application nyingine kibao kama nyenzo ya mawasiliano.



Kadiri siku zinavyosonga, suala la sauti ambalo lilionekana liko juu zaidi linakwenda kuzidiwa nguvu na suala la sauti na mwonekano kwa maana ya video.

Video ndio zinazoaminika zaidi, kwamba anazungumza anasikika na anaonekana.Ushahidi wa video unachukua uaminifu mkubwa kwa wahusika wanaokuwa wanazungumzia jambo fulani.

Ndio maana umeona suala la mjadala ulioanzishwa na Haji Manara, msemaji wa Yanga ukiisha haraka sana kwa kuwa teknolojia imemhukumu.

Teknolojia imemhukumu Manara kupitia yeye mwenyewe. Hakuna yoyote katikati yake ameweka maneno. Zaidi amezungumza yeye na akajijibu yeye.

Mjadala aliouamsha ni kwamba Yanga ndio klabu yenye makombe mengi zaidi iliyoshinda katika michuano mbalimbali.

Wakati anayasema hayo, tayari yalikuwa yanapingwa na wadau wengi wa mpira ambao wanajua Simba ndio ina makombe mengi.

Wadau hao wamekuwa na sehemu nyingine ya uthibitisho ingawa, uthibitisho wa uhakika zaidi wao wameutumia ni wa Manara mwenyewe. Maneno ambayo aliyazungumza miezi kadhaa tu iliyopita.

Katika hauli hiyo, Manara wakati akihojiwa na Baruan Muhuza wa Azam TV alisema kwamba Simba ndio yenye makombe mengi zaidi akijaribu kutoa ufafanuzi kadhaa.

Bahati nzuri sana, hakuna aliyempinga wakati ule kwa kuwa limekuwa ni jambo lililokuwa likijulikana licha ya kuwepo na mkinzano wa idadi sahihi ya Simba kachukua mangapi na Yanga anayo mangapi.


Safari hii kungeweza kuwa na ubishi mkubwa, kwa kuwa Manara amezungumza kitu tofauti na kinachofahamika lakini bahati mbaya zaidi, teknolojia inakwenda kuwa kigezo cha kumrudisha nyuma katika kauli yake hiyo.


Bahati mbaya zaidi, anayetumika kumzima Manara kutokana na alichokisema ni Manara mwenyewe. Kwamba Simba ndio kubwa zaidi kama ukisema suala la makombe mengi zaidi iliyobeba.


Video ya Manara akisema Yanga ndio ina makombe mengi zaidi na Simba ina makombe mengi zaidi, zimeunganishwa.

Zote anaonekana na kusikika Manara akisema, hakuna mtu mtu mwingine.Kunakuwa hakuna ubishi kwa kuwa anayezungumza ni Manara na anayemjibu ni Manara. Haya yote ndio sehemu ya kuonyesha kiasi gani teknolojia inapiga hatua kwa kasi kubwa.


Unaweza kusema kama ni ubishi, wanaobishana ni akina Manara na Manara mmoja anampinga mwingine. Lakini haya yote ni kutokana na namna teknolojia ilivyopiga hatua.


Achana na yale mambo ya kishabiki, hapa piga hesabu ya teknolojia yenyewe na ujue inatufundisha mambo mengi sana hasa kwa wale wenye uwezo wa kufanya jambo au mambo mbele ya jamii.


Kwamba siku zijazo zinaweza kushikiliwa na zile zilizopita kulingana naulichokizungumza. Hivyo ni vizuri sana kuwa makini maradufu kwa kila unachokizungumza leo.

Kama hautakuwa makini, hakutakuwa na mtu mwingine, badala yake wewe mwenyewe kupitia teknolojia utakinzana na wewe mwenyewe na mwisho utashindwa na wewe mwenyewe.


Ndio maana nikasema kilichotokea kuanzia jana kuhusiana na alichokisema Manara na baadaye kujibiwa na alichowahi kukisema,maana yake ni funzo ambalo hatupaswi kuona limemtokea Manara tu. 

Badala yake hata wewe na mimi kama tunachozungumza hatutakuwa nacho makini, kitatuangusha katika siku za usoni.


Saleh Ally

11 COMMENTS:

  1. Wewe na Haji mpo sawa ,hata wewe unazi wa Simba inafika hatua mnafunika mnasahau maadili ya kazi yenu hayo ndiyo matokeo yake.Najua unamia enzi zake yupo Simba ulikuwa unatoa makala ndefu ku support upande wake.

    ReplyDelete
  2. Mtu akizungumza ukweli eti
    nu mnazi wa Simba.jitu likiwa laghai,muongo mpaka anaidanganya nafsi yake mwenyewe ilimradi yupo Yanga Basi ni mkweli. Kama ningekuwa nina Maamuzi ndani ya Yanga ningemfukuza Manara mchana kweupe hana credibility. Manara hajaaja kuimarisha Yanga isipokuwa amekuja kuizofisha Yanga kimaadili.Hata yale madai ya Manara kuwa alikuwa akionewa Simba sijui aa ni watu wabaya sasa inajiweka wazi yenyewe kuwa Manara ni Muongo na ndio maana alishindwa kwenda kwenye vyombo vya sheria kuthibitisha madai hayo kwakuwa Manara alijua kuwa madai hayo sio ya ukweli.

    ReplyDelete
  3. Wewe unataka kueleza Nini ,Watu wa media mna miiko na maadili yenu ya kazi,na hii inazidi kutufungua kujua ukweli wa taaluma yenu hususani Tanzania kwanza mmekuwa mkitumika kwa interest zenu na za watu wenu , mlisajili blog,TV,Redio na kuzitumia Kama uwanja wa kutoa hisia zenu Binafsi na mmekwenda zaidi ninyi mnajua kila kitu eg Utawala,kucheza,siasa na kila kitu ninyi mpo juu ya kila mtu kisa Waandishi wa habari mnamfikia kila mtu na mpo tayari kupotosha jamii ili mradi lenu lipite.Maana huyu mtu tumempigia kelele uadirifu wake alipo kuwa upande wenu mlikuwa hata akiitisha press mnaogopa kumuuliza au mna support na kumsifia anavyo dictate press cse mpo mlengo mmoja.Na hiyo Timu kwenye hivi vyombo vingi hususani Fm Redio,TV,na blog wengi Waandishi wanazi ile Wasafi kipindi Cha michezo jioni 50 dk wanaongelea Timu moja mpaka wakienda kinyume msemaji anaingilia kipindi anapiga Simu.Ligi ya mwaka Jana imeendeshwa kihuni imechukua muda mrefu kisa inakuwa favoured Timu moja I accomplish mission,lkn hakuna sehemu moja mnaeleza hathari zake kwa huu msimu na kulaumu TFf ,Sana mnafurahia kuwa Viongozi waliovurunda ndiyo hao wapo hata leo.Ratiba tu inawashinda.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nyoosha maneno maana hueleweki ndugu. Manara anahitaji maombi maana kwa kweli ameharibikiwa pakubwa

      Delete
    2. Kweli kabxa,, nashauri apelekwe kwa askofu gwajima haraka sn! Haa haaa

      Delete
  4. Huyu jamaa Kocha yeye, Mwandishi yeye, Msemaji yeye,mpaka anasahau anatukana Mwajiri wake.Lakini akina Salehe Ally wamekuwa wakifurahia habari zake ilimradi yupo upande wao ,Sasa hivi ndipo wanamgundua kuwa alikuwa na agenda ndani ya Mpira siyo mapenzi.Hawa watu wanajiita wa Mpira hawafai utakuta hata Uwanjani wanaingia bure(complementary)wengine wakitegemea mgao kwenye viingilio,sisi huku tuna humia wenzetu wanaangalia kaingiza Nini.Kakangu alicheza naye Simba Kids .

    ReplyDelete
  5. mwanadamu ana kawaida hiyo.hiyo ni sifa mojawapo ya wanadamu.sio haji manara tu kwenye siasa.michezo,na kila nyanja.viongozi wetu leo na misimamo yao,ni tofauti kabisa na ile waliyokua nayo mwaka mmoja uliopita.mmoja alisema tusiwafate wazungu,sie tupige nyungu,alipofariki rais,akatweet tunaamini ujinga na kudharau sayansi.na wengine wengi.ila wengi wetu tabia hii ya kigeugeu huifanya ktk ngazi ya familia ama mtaa,ila haji anaifanya kitaifa,uzuri anatahadharisha maneno sio msahafu wala biblia.demu wako wa zamani ulimwambia unampenda kuliko chochote,na mkeo leo unamwambia hivyohivyo.na mchepuko pia hivyohivyo.hii dunia ni ya kina haji.ile wengi ni ngazi ya kitongoji.

    ReplyDelete
  6. Yaani wewe ndo umetoa ufafanuzi zaidi Lakini kwa interest ya public watu wajifunze maadili cse issue nyingine effect zake Zina hathiri jamii kubwa na zipo kwa ajili ya Jamii kwa maana zimeanzishwa kujenga ustaarabu wa kuishi na kutegemeana kila mmoja na Jukumu lake ,kwa ufafanuzi zaidi Professional yake.Ya Familia au mpenzi impact yake Ni kwa level Ile watu wachache,lkn level ya Waziri(Public figure) ?neno lenyewe Waziri ,Mwandishi na Mpenzi tafsiri yake kwa maana ukitafsiri Ni Mtu wa aina gani na wajibu wake utasema siyo watu wa majukumu sawa .Tuangalie kwa nafasi zao na kwa mahitaji na utambuzi wao kwenye Jamii tujiulize level ya uadirifu ituongoze .Kiongozi akiwa mwongo wanaathirika wangapi?

    ReplyDelete
  7. Wengi hulinda mfuko hawalindi mdomo, ambao unaleta matokeo hasi au chanya yasio tarajiwa, mfuko unaweza kuleta matokeo tarajiwa kwa % kubwa. Kwa kiasi kikubwa mdomo umeumiza watu wengi na kubwa na maumivu makubwa mbaya zaidi wengine walikufa ama kujinyonga kwa hilo. Self assessment he wewe umemuuza nani halo ulipo. Je waweza rekebisha palipo haribika kwa mdomo wako. Toba MUHIMU

    ReplyDelete
  8. Wengi hulinda mfuko hawalindi wala kujizuia kuutumia ulimi wao vyema ( no self discipline) ambao pasipo kuwa na kiasi ulimi huleta madhara makubwa kwa wengine. Tumeumiza wengi katika mahusiano yetu, na mahangaiko yetu ya maisha. Ubinadamu ni kumjali mwingine tafsiri sawia ya utu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic